Pata taarifa kuu
KENYA-TANZANIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Wavuvi 16 kutoka Tanzania washikiliwa Kenya

Maafisa wa usalama nchini Kenya, wanashikilia wavuvi 16 kutoka nchini Tanzania, wanaodaiwa kuvuka mpaka na kutumia vifaa visivyoruhusiwa kuvua katika Ziwa Victora.

Boti la uvuvi kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda.
Boti la uvuvi kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda. Damiano Luchetti/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Wavuvi hao wamekamatwa karibu na fukwe ya Bamgot, katika Kaunti ya Migori kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa eneo hilo, Joseph Nthenge ambaye amesema washukiwa watapelekwa Mahakamani.

Wavuvi kutoka Kenya, Tanzania na Uagnda, nchi zinazotumiwa maji ya Ziwa Victoria kwa pamoja, wamekuwa wakitoa wito kwa serikali za nchi hizo za Afrika Mashariki, kuweka mipaka inayoonekana ili kuepuka kukamatwa mara kwa mara.

Wiki kadhaa zilizopita, polisi wa Tanzania waliwakamata wavuvi 36, kwa madai ya kuvua katika maji yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.