Pata taarifa kuu
KENYA-RIADHA-KIFO

Kenya yaomboleza kifo cha mwanariadha Nicholas Bett

Kenya inaomboleza kifo cha mwanariadha Nicholas Bett,  bingwa wa mwaka 2015 wa mashindano ya riadha ya dunia katika mbio za Mita 400 kwa upande wa wanaume.

Marehemu Nicholas Bett aliposhinda mbio za Mita wakati wa mashindano ya riadha ya dunia jijini Beijing nchini China mwaka 2015
Marehemu Nicholas Bett aliposhinda mbio za Mita wakati wa mashindano ya riadha ya dunia jijini Beijing nchini China mwaka 2015 AFP
Matangazo ya kibiashara

Bett amepoteza maisha baada ya kupata ajali katika barabara ya kutoka mjini Eldoret kwenda Kapsabet katika kaunti ya Nandi, Jumatano alfajiri.

Wanariadha na wapenzi wa riadha nchini humo wameguswa na kifo cha mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alishiriki katika mashindano ya Afrka yaliyomalizika Jumapili iliyopita mjini Assaba nchini Nigeria.

Bett, alilazimika kujiondoa katika fainali ya mbio za Mita 400 baada ya kupata jeraha mita 200 tu baada ya kuanza mbio hizo.

Ripoti zinasema kuwa, mwanariadha huyo alipata ajali hiyo wakati akienda kumwona rafiki yake baada ya gari lake kugonga tuta na kubingiria mara kadhaa.

Atakumbukwa kuwa mwanariadha wa kwanza kutoka nchini Kenya kushinda taji hilo la mbio za Mita 400, kuwahi kushinda mbio hizo fupi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.