Pata taarifa kuu
SUDANI-KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Salva Kiir na Riek Machar kukutana tena Khartoum

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wanatarajia kukutana tena Khartoum, nchini Sudani Jumatatu wiki ijayo kwa mkutano wao wa pili wa mazungumzo.

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (D) akimshika mkono hasimu wake Riek Machar wakati wa mkutano huko Ethiopia Juni 21, 2018.
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (D) akimshika mkono hasimu wake Riek Machar wakati wa mkutano huko Ethiopia Juni 21, 2018. Presidential Press Service/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hawa wanaendelea kukutana kwa lengo la kupata suluhisho la vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao.

Mazungumzo hayo, ambayo yanafuata mkutano wa kikanda wa mataifa ya Afrika Mashariki nchini Ethiopia ili kufufua mchakato wa amani nchini Sudani Kusini, yatafanyika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umetoa muda hadi mwishoni mwa mwezi Juni kwa makundi hasimu kuwa yamefikia " mkataba wa kisiasa unaofaa ", huku ukitishia kuwachukulia vikwazo.

Rais wa Sudani Omar al-Bashir anatarajia kuwa msimamizi wa mazungumzo hayo ya moja kwa moja kati ya viongozi hawa wawili wa Sudani Kusini mnamo Juni 25 mjini Khartoum, "Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudani imesema katika taarifa yake.

Sudani itafanya kila kilio chini ya uwezo wake ili makundi hasimu nchini Sudani Kusini yafikie makubaliano ya kudumu, Wizara hiyo imeongeza.

Timu ya kiufundi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki (Igad), inayoendelea na jitihada za kuimarisha mchakato wa amani nchini Sudani Kusini, itawasili Khartoum mwishoni mwa wiki hii, chanzo hicho kinasema.

Sudani Kusini ilipata uhuru kutoka Sudani mwaka 2011. Nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa mwaka 2013 wakati Kiir alimshtumu makamu wake wa zamani, Riek Machar, kujaribu kumpindua madarakani.

Mgogoro uliosababishwa na wawili hao umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamilioni ya watu kuyatoroka makaazi yao. Mamia ya maelfu wamekimbilia nchini Sudani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.