Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-SIASA-USALAMA

Salva Kiir kukutana na kiongozi wa waasi Riek Machar Jumatano hii

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anatarajia kukutana na hasimu wake, Makamu wa zamani wa rais Riek Machar Jumatano wiki hii kujadili namna ya kuanzisha upya mchakato wa amani unaotarajiwa kumaliza mgogoro unaoikabili nchi hiyo tangu mwaka 2013, kwa mujibu wa serikali ya Ethiopia.

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kushoto) na kiongozi wa waasi Riek Machar (kulia).
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kushoto) na kiongozi wa waasi Riek Machar (kulia).
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wamewasili Jumatano wiki hii Addis Ababa, Ethiopia ambako watakutana kwa mara ya kwanza tangu miaka miwili iliyopita, katika kujaribu kuleta amani katika nchi yao iliyoharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013 .

Mgogoro huu, ambao ulizuka mnamo mwezi Desemba 2013 kwa sababu ya uhasama kati ya wawili hawa, umesababisa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, uliosababisha  vifo vya maelfu ya watu, huku watu karibu milioni nne wakiyatoroka makazi yao na kusababisha janga kubwa la kibinadamu.

Mkutano huu kuhusu Sudan Kusini utafanyika chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu (Ethiopia) Abiy Ahmed ili kuzuia pengo kati ya Rais Salva Kiir na Riek Machar," Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema.

Nakala hiyo inaongeza kuwa Riek Machar anatarajiwa Addis Ababa Jumatano wiki hii.

Awali serikali ya Sudani Kusini ilitaka mkutano wa ana kwa ana kati ya rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar ufanyike katika taifa lisilo na maslahi na upande wowote kati ya viongozi hao.

Siku ya Jumatatu wiki hii Waziri wa habari na msemaji wa serikali ya Juba Michael Makuei, alisema mkutano wa kihistoria unaweza kufanyika katika taifa lolote kutokana na kuwepo mvutano wa kimaslahi miongoni mwa mataifa ya jumuiya ya iGAD ambayo yamekuwa yakiandaa mazungumzo hayo.

Miongoni mwa mataifa ambayo yamewahi kuandaa mazungumzo hayo ni pamoja na Ethiopia na Kenya lakini hivi karibuni na Sudani ya khartoum nayo ilitangaza kuwa tayari kuandaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.