Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNSC-USALAMA-SIASA

UNSC yagawanyika kuhusu hali inayoendelea Burundi

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Michel Kafando, ametoa wito wa kufufua upya mazungumzo baina ya Warundi, njia pekee, amesema, itakayokomesha mgogoro nchini humo tangu mwaka 2015. Lakini wanadiplomasia wamenekana wakigawanyika kuhusu jinsi ya kuimarisha nchi hiyo.

Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York (picha ya kumbukumbu. Moscow imesisitiza kuwa suala la Burundi halingepaswa tena kuepo kwenye ajenda  kikao cha baraza hilo.
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York (picha ya kumbukumbu. Moscow imesisitiza kuwa suala la Burundi halingepaswa tena kuepo kwenye ajenda kikao cha baraza hilo. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo inakuja siku nne baada ya kupitishwa kwa mageuzi ya katiba ambayo yatamruhusu rais Pierre Nkurunziza kuendelea kukaa madarakani kwa miaka zaidi yakumi na nne, Michel Kafando ametoa kauli hiyo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika siku ya Alhamisi wiki hii .

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, bado ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa? "Ndiyo," ameijibu mjumbe wa Ulaya kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambaye amesema kuwa kura ya maoni iliyofanyika nchini humo ilikua kinyume na mkataba wa amani na usalama wa Arusha na hivyo kusababisha hatari ya kudorora kwausalama usalama.

Hata hivyo serikali ya Bujumbura inaungwa mkono na vigogo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Urusi na China, wanachama wawili wa kudumu wenye kura ya veto. Moscow imesisitiza kuwa suala la Burundi halingelipaswa kuepo tena kwenye ajendaya kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini mikononi mwa idara maalum za Umoja wa Mataifa. China, Bolivia na Equatorial Guinea, zote tatu zili sisitiza juu ya umuhimu wa Burundi kutumia huru wake wa kufanya kura ya maoni.

Kwa upande wa mashirika ya kimataifa ambayo yanafuatilia kwa karibu kufuata hali inayoendelea nchini Burundi, wanasema shinikizo la kimataifa halitoshi kabisa na Burundi inaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kikanda na pia kwa uaminifu wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo kuna ukosefu wa maelewano kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hali ambayo inaendelea kumpa nguvu rais Nkurunziza kubaki kiongozi wa ngazi ya juu wa mustakabali wa nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.