Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-JESHI-VIKWAZO

Rais Kiir amfuta kazi kiongozi wa juu wa jeshi na Waziri wa fedha

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amemfuta kazi mmoja wa viongozi wa juu wa jeshi nchini humo Luteni Jenerali Marial Chanuang Yol Mangok.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Hadi kufutwa kwake kazi, Jenerali Mangok amekuwa Naibu Mkuu wa jeshi katika taifa hilo ambalo limeendelea kushuhudia vita kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Jenerali Mangok ni mmoja wa Majenerali sita waliowekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa mwaka 2015 kwa sababu ya kuchochea kuendelea kwa mauaji nchini humo.

Mwaka uliopita, rais Kiir alimfuta kazi aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Paul Malong baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuwa jeshi la serikali limekuwa likiwauwa raia wasiokuwa na hatia.

Mbali  na hilo, rais Kiir amemfuta kazi Waziri wa fedha Stephen Dhieu Dau.

Rais Kiir hakutoa sababu yoyote ya kufikia maamuzi hayo.

Wiki iliyopita, Shirika la Kimataifa la Crisis Group lilitoa ripoti ya kuituhumu serikali ya Sudan Kusini kutumia biashara ya mafuta kununua silaha na kuwalipa wanajeshi ili kuendelea kwa vita nchini humo.

Hivi karibuni, Marekani inatarajiwa kuwasilisha azimio la kutaka serikali ya Sudan Kusini kuwekewa vikwazo vya kununua silaha nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.