Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini kumalizika Ijumaa

Kikao cha mwisho cha mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yanayosimamiwa na Ethiopia kinaweza kumaliza leo Ijumaa kwa kufikia makubaliano ya kusitishwa kwa vita, mjumbe wa Umoja wa Mataifa David Shearer amesema.

Mgogoro unaosababishwa na machafuko ya kikabila umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na karibu watu milioni nne kuyatoroka makazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.
Mgogoro unaosababishwa na machafuko ya kikabila umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na karibu watu milioni nne kuyatoroka makazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu. REUTERS/David Lewis
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo, ambayo yalianza Februari 5 mjini Addis Ababa, yana lengo la kupata suluhisho la mojawapo ya migogoro mabaya zaidi barani Afrika.

"Tunatumaini kuwa kutakuwa na aina ya makubaliano yatakayosainiwa kesho (Ijumaa)," Shearer aliwaambia waandishi wa habari. "Inawezekana mkataba huo ukachelewa kuliko tulivyotarajia, lakini hali hiyo inaweza kutoa aina ya majadiliano."

Majadiliano nchini Ethiopia yalijikita kuhusu utawala na usalama.

Umoja wa Afrika na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametishia kuweka vikwazo dhidi ya wale wanakwamisha juhudi za amani nchini Sudan Kusini.

Sudan Kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwezi Desemba 2013 wakati Rais Salva Kiir alimshtumu makamu wa rais wa zamani Riek Machar kupanga mapinduzi dhidi ya serikali.

Mgogoro unaosababishwa na machafuko ya kikabila umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na karibu watu milioni nne kuyatoroka makazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.