Pata taarifa kuu
MAREKANI-KENYA-SIASA

Marekani yaelezea wasiwasi wake kuhusu Kenya

Siku tatu baada ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kujiapisha mwenyewe, Marekani imeleelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Kenya.

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga, Novemba 28, 2017.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga, Novemba 28, 2017. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo kutoka wizara ya mambo ya Nje ya Marekani, tukio la hivi karibuni nchini Kenya la kiongozi wa upinzani aliyeshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi na kisha kususia uchaguzi mpya wa duru ya pili linaonesha kuwa hali si nzuri nchini humo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hearther ameinyoonshea kidole cha lawama seikali ya Kenya kwamba imekataa kuketi na upinzani kwa lengo la kutafutia ufumbuzi kwa pamoja mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Aidha, mesema malalamiko kuhusiana na uchaghuzi nchini Kenya yanapaswa kutatuliwa kupitia utaratibu unaofaa wa kisheria.

ambako kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alijiapisha mwenyewe kuwa ''Rais wa Wananchi'' siku ya Jumanne.

Hearther Nauerth aameishtumu pia serikali ya Kenya kwa uamuzi wake wa kuvifungia vituo vitatu vya serikali, baada ya kurusha matangazo ya moja kwa moja tukio hilo la kujiapisha kwa Raila Odinga

Raila Odinga alijiapisha mwenyewe kuwa ''Rais wa Wananchi” siku ya Jumanne Januari 30, 2017. Sheree ambayo serikali ilikua ilipiga marufuku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.