Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Fred Matiang'i: Raila alilenga kuipindua serikali

Waziri wa Mambo ya ndani nchini Kenya, Fred Matiang'i amesema kitendo cha kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kujiapisha siku ya Jumanne kama rais wa watu, kililenga kuipindua serikali.

Raïla Odinga, kiongozi wa upinzani, wakati akiapishwa, Januari 30, 2018 Nairobi.
Raïla Odinga, kiongozi wa upinzani, wakati akiapishwa, Januari 30, 2018 Nairobi. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Waziri huyo amesema vyombo vya Habari vilivyozimiwa mitambo, vitaendelea kuwa hivyo hadi uchunguzi utakapomalizika baada ya kuvizuia kuonesha kiapo cha Odinga.

Wakili TJ Kajwang aliyemwapisha Odinga amekamatwa kwa uchunguzi zaidi huku baadhi ya wabunge wa muungano wa NASA wakisema serikali imewapokonya walinzi wao.

Raila Odinga, mwanasiasa wa upinzani kwa miaka mingi nchini, aliapishwa siku ya Jumanne kama rais wa wananchi wa Kenya, baada ya siku nyingi kutishia kufanya hivyo.

Odinga ambaye alishindwa katika uchaguzi wa urais mwaka jana, katika hotuba yake alibaini kwamba aliamua kufanya hivyo baada ya kuonekana kuwa angelishinda uchaguzi wa kwanza kama haengelikua wizi wa kura. Aliishtumu Tume ya Uchaguzi ya Kenya IEBC kuhusika katika udanganyifu huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.