Pata taarifa kuu
KENYA-AJALI

Watu 36 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani nchini Kenya

Watu 36 wamepoteza maisha na 11 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani nchini Kenya iliyotokea mapema siku ya Jumapili.

Ajali ya basi na Lori nchini Kenya
Ajali ya basi na Lori nchini Kenya PHOTO | FRANCIS MUREITHI | NATION MEDIA GROUP
Matangazo ya kibiashara

Polisi wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kugongana ana kwa ana kwa basi la abiria na lori, katika eneo la katikati ya nchi hiyo.

Mkuu wa kitengo cha trafiki katika eneo la Bonde la Ufa,  Zero Arijme, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo amesema ilitokea saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya kutoka Nakuru kwenda mjini Eldoret.

Basi la abiria lilikuwa limetokea mjini Busia, mpakani na nchi ya Uganda kuelekea jiji kuu la Nairobi wakati lilipogongana na lori lililokuwa limetoka mjini Nakuru.

Polisi nchini Kenya wanasema mwezi wa Desemba pekee, watu 100 wamepoteza maisha katika ajali za barabarani zilizotokea katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.