Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-USALAMA

Diane Rwigara kufikishwa mahakamani Ijumaa

Mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara anatarajiwa kufikishwa Mahakamani siku ya Ujumaa Oktoba 6, 2017.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, mmoja wa waliotaka kuwania kiti cha urais nchini humo Diane Rwigara.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, mmoja wa waliotaka kuwania kiti cha urais nchini humo Diane Rwigara. REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja siku moja baada ya kutuhumiwa kughushi nyaraka muhimu wakati wa mchakato wa kuwatafuta wagombea urais mwezi Agosti, lakini pia anashtumiwa kwa kudharau mamlaka ya nchi.

Rwigara mwenye umri wa miaka 35, ameshikiliwa yeye na ndugu zake wa karibu jijini Kigali na amekuwa akikanusha madai dhidi yake.

Polisi nchini Rwanda imeendelea kuwa kwenye shinikizo zaidi kutoka kwa familia ya aliyekuwa mmoja wa waliotaka kuwania kiti cha urais nchini humo Diane Rwigara ambaye awali alidaiwa kushikiliwa na vyombo vya usalama.

Hivi karibuni Uingereza ilikosoa vikali serikali ya Rwanda kwa kunyanyasa na kukamata wanasiasa wa upinzani tangu uchaguzi wa urais wa Agosti 4, ambapo rais anayemaliza muda wake Paul Kagame aliibuka msindi kwa 99% ya kura.

Awali polisi ilimtuhumu Diane Rwigara na ndugu zake kuwa na "uhusiano na makundi ya waasi yanayoendesha harakazi zao katika nchi jirani", ikimaanishwa Kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda la FDLR nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.