Pata taarifa kuu
KENYA-AJALI

Waandishi wa habari wanasurika baada ya ndege yao kuanguka Kenya

Ndege ndogo aina ya Cessn iliokuwa ikiwabeba waandishi wa habari ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa Wilson Airport mjini Nairobi, nchini Kenya, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.

Ndege ya mizigo iliogonga majengo baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa Nairobi, Kenya, Julai 2, 2014..
Ndege ya mizigo iliogonga majengo baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa Nairobi, Kenya, Julai 2, 2014.. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Daily Nation limesema kuwa kamanda wa polisi wa kitengo cha angani Rodgers Mbithi alithibitisha ajali hiyo na kubaini kwamba waandishi hao na wafanyakazi wa ndege hiyo hali yao inaendelea vizuri.

Maripoa wawili na mpiga picha mmoja kutoka kituo cha televishwni cha Citizen walikua wakisafiri wakielekea kutafuta habari za muungano wa Upinzani NASA katika eneo la Baringo.

Dakika chache baada ya ajali hiyo waandishi hao na wafanyikazi wa ndege hiyo walipelekwa katika hospitali ya Nairobi.

Mapema siku ya Ijumaa ndege ya Canada nusura igonge ndege nne uwanjani San Francisco.

Idara inayohusika na safari za ndege nchini Marekania FAA inasema kuwa ndege ya AC759 ikitokea Toronto iliruhusiwa kutua siku ya Ijumaa lakini rubani akajianda kutua katika barabara ambapo ndege zingine zilikuwa zinajianda kupaa.

Waelekezi wa safari za ndege waliweza kufahamu tatizo hilo na kumuamrisha rubani kupaa tena ili kujiandaa kutua kwa kwa mara ya pili.

Mapema mnamo mwezi Julai 2014 ndege ya mizido Ndege ya mizigo iligonga majengo baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa Nairobi, nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.