Pata taarifa kuu
KENYA-TANZANIA

Kenya na Tanzania zatangaza vita dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya

Serikali ya Kenya na Tanzania, zimetangaza vita dhidi ya walanguzi na watumiaji wa dawa za kulevya katika nchi zao.

Watumizi wa dawa za kulevya
Watumizi wa dawa za kulevya
Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki yanaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya biashara hiyo katika miji ya Pwani hasa jijini Dar es salaam na Mombasa.

Wiki iliyopita, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alitangaza majina ya washukiwa wa biashara hiyo wakiwemo maafisa wa polisi, wasanii maarufu na watu wengine na kuwataka kufika polisi ili kuhojiwa.

Hatua hii imeungwa mkono na rais wa nchi hiyo John Magufuli ambaye amesema hakuna atakayeachwa katika vita hivi.

“Katika vita hivi vya dawa za kulevya, hakuna cha mtu maarufu, hakuna cha mwanasiasa, askari, Waziri au mtoto wa fulani, hata angekuwa mke wangu Janet amehusishwa, akamatwe tu,” alisema rais Magufuli.

Polisi wanaoshukiwa kuhusika katika biashara hii tayari wamesimamishwa kazi wakati huu uchunguzi ukiendelea.

Hali kama hii inashuhudiwa nchini Kenya, baada ya serikali kuwasafirisha nchini Marekani washukiwa wanne  Ibrahim Akasha Abdalla, Gulam Hussein, Vijaygiri Anandgiri Goswami na Baktash Akasha Abdalla kufunguliwa mashtaka ya kuhusika na biashara hii.

Naibu rais William Ruto akiwa ziarani mjini Mombasa, amesema siku za walanguzi wa dawa za kulevya zimefika mwisho.

“Kenya haina nafasi ya walanguzi wa dawa za kulevya, watafute nchi nyingine ya kwenda, Kenya hapakaliki,” alisema Ruto.

Kenya na Tanzania kwa muda mreefu imekuwa ikipambana na biashara hii haramu ambayo imewaharibu maelfu ya vijana hasa katika Pwani ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

Inashukiwa kuwa biashara hii imekuwa vigumu sana kumaliza biashara hii katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sababu inawahusisha watu wenye ushawishi kama wanasiasa na watu wengine wenye utajiri wa fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.