Pata taarifa kuu
TANZANIA-JAMII-MAENDELEO

Rais Magufuli azindua daraja mpya Kigamboni-Dar

Rais wa Tanzania John Magufuli amezindua daraja mpya la Kigamboni jijini Dar es salaam lenya urefu wa Kilimota 680 inayounganisha eneo la Kurasini na Kigamboni.

John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015.
John Pombe Magufuli, Rais mpya wa Tanzania, Oktoba 30, 2015. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Daraja hilo ambalo limepewa jina la Nyerere, mwanzilishi wa taifa hilo liligharimu Dola za Marekani 128 kwa msaada wa serikali ya China.

Akizundua daraja hilo, rais Magufuli ameeleza kuwa watumiaji wa daraja hilo hasa wale walio na pikipiki, baskeli na magari watalipia lakini wale wanaotumia miguu watapita bure.

Katika hatua nyingine, rais Magufuli amewaambia Watanzania kuwa ataendelea kuwachukulia hatua wafanyikazi wa serikali ambao hawawajibiki iapsavyo kazini.

Amewataka watumishi wa Umma wasioweza kuendana na kasi yake waondoke.

Daraja mpya linalounganisha Dar es Salaam-Kigamboni.
Daraja mpya linalounganisha Dar es Salaam-Kigamboni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.