Pata taarifa kuu

Tanzania: Kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani linaendelea

Nairobi – Nchini Tanzania, Jumatatu ya wiki hii kulizinduliwa kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani, ambapo waziri mkuu wa nchi hiyo, Kassim Majaliwa, akiwataka wadau kutumia fursa ya Kiswahili kama ajira kwa mataifa ya kigeni.

Wadau wa Kiswahili wanakutana nchini Tanzania.
Wadau wa Kiswahili wanakutana nchini Tanzania. © BAKITA
Matangazo ya kibiashara

Kutoka Mbeya, Tanzania, mwanahabari wetu Ali Bilali alituwakilisha na kututumia ripoti ifuatayo.

Wadau kwenye kongamano hilo wanapokea ripoti ya uswasilishaji wa maazimio ya makongamano yaliyopita.

Wadau wa Kiswahili  kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania wanakutana kujadili masula mbalimbali kuhusu lugha hii.
Wadau wa Kiswahili kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania wanakutana kujadili masula mbalimbali kuhusu lugha hii. © BAKITA

Gerison Msigwa ni katibu mkuu kwenye wizara ya utamaduni Sanaa na michezo.

‘‘Mkutano kama huu ndio unatusaidia sana sisi kama wadau kuona ni namgana Kiswahili kinazungumzwa kwa ufasaha.’’ alisema Gerison Msigwa. 

00:09

Gerison Msigwa ni katibu mkuu kwenye wizara ya utamaduni Sanaa na michezo

kwenye kongamano hilo ambalo wadau wanajaribu kunyoosha kiswahili, lakini Bi Idda Sanga mwandishi mkongwe wa habari kutoka nchini Tanzania anasema hali ya Sasa ni tofauti kabisa na zama zao.

‘‘Leo hii kwa kweli Kiswahili kimeporomoka kwa sababu kinatumika hata Kiswahili cha mtaani kinakuja kuwa rasmi katika utangazaji.’’ alieleza Bi Idda Sanga.

00:13

Bi Idda Sanga mwandishi mkongwe wa habari

Lakini sasa nini kifanyike kurekebisha hali hiyo, Dkt Onesmo S. Nyinondi ni mhadhiri katika chuo kikuu cha kilimo mjini Morogoro.

‘‘Miongozo na tasisi za elimu zinapashwa kuendelea kuelimisha umma.’’ alisema Dkt Onesmo Nyinondi.

00:05

Dkt Onesmo Nyinondi

Kwa muda wa siku 5 wadau kutoka katika Kila Kona ya Tanzania na nje ya Tanzania, watajadili na kutathimi maazimio ya kongomano la mwaka jana na baadae kuunda mbinu na mikakati ya kuifanyia kazi.

Ali Bilali- Mbeya RFI-Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.