Pata taarifa kuu

DRC: Rais Tshisekedi ameonyesha nia ya kukutana na mwenzake wa Rwanda

Nairobi – Mkutano kati ya Paul Kagame na Félix Tshisekedi utafanyika hivi karibuni kujaribu kutatua mgogoro kati ya nchi hizo mbili.

kinshasa ina matumaini kuona Umoja wa Afrika unatumia vema jukumu lake katika mchakato wa amani
kinshasa ina matumaini kuona Umoja wa Afrika unatumia vema jukumu lake katika mchakato wa amani AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya kila upande Rwanda na DRC kuonyesha dhamira ya kutaka kuzungumzia kina cha mgogoro huo kulingana na taarifa kutoka nchini Angola ambayo ndio inajaribu kupatanisha pande hizo mbili.

Jijini Kinshasa, watu wa Karibu na rais Felix Thisekedi wanathibitisha nia ya dhati ya rais Felix Tshisekedi ya kutaka kukutana na rais wa Rwanda Paul Kagame.

Hata hivyo wameweka wazi masharti yaliowekwa na serikali ya Kinshasa Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, kama ilivyotolewa wito na Jumuiya kimataifa kuondoa vikosi vya Rwanda katika ardhi ya Congo pamoja na vifaa vyake.

Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamekuwa wakitafuta suluhu ya kinachoendelea mashariki ya DRC.
Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamekuwa wakitafuta suluhu ya kinachoendelea mashariki ya DRC. © RDC

Hili ni moja ya sharti lilitolewa kabla ya mkutano huo wa ana kwa ana kati ya marais hao wawili.Sharti lingine lilitolewa ni pamoja na M23 kuondoka katika maeneo walioyateka hivi karibuni, ombi ambalo lilitolewa na kuungwa mkono na baraza la usalama la Umoja wa Afrika.

kinshasa ina matumaini kuona Umoja wa Afrika unatumia vema jukumu lake katika mchakato wa amani.

Ni katika dhamira hiyo, rais Felix Tshisekedi amewasiliana hivi majuzi kwa njia ya simu na rais wa Mauritania Muhamed Ould Gazwani ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika kuzungumzia swala hili muhimu na kuonyesha jukumu la Umoja wa Afrika katika kutafuta suluhu, kama walivyothibitisha mabalozi wa mataifa ya magharibi jijini Kinshasa.

Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaotatiza usalama mashariki mwa DRC.
Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaotatiza usalama mashariki mwa DRC. © afp:Tchandrou Nitanga

Baraza la usalama la Umoja wa Afrika limepewa jukumu la kuandaa mkutano hivi karibuni utaojumuisha viongozi wa Jumuiya ya Afrika mashariki, jumuiya ya nchi za Afika ya kati na Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.