Pata taarifa kuu

Zanzibar: Watu tisa wamefariki baada ya kula nyama ya kasa

Nairobi – Katika kisiwa cha Pemba, visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania watoto wanane na mtu mzima mmoja wamepoteza maisha baada ya kula nyama ya kasa huu watu wengine 78 wakikimbizwa hospitalini.

Mamlaka visiwani Zanzibar, imewataka watu  kuepuka kula kasa wa baharini.
Mamlaka visiwani Zanzibar, imewataka watu  kuepuka kula kasa wa baharini. © CC/Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Nyama ya kasa wa baharini inachukuliwa kuwa ni tamu sana visiwani Zanzibar lakini mara kwa mara husababisha vifo kutokana na chelonitoxism, aina ya sumu inayopatikana katika samaki huyo asipotengenezwa vizuri.

Kwa mujibu wa mganga mkuu wa wilaya ya mkoani dokta Haji Bakari amesema aliyefariki dunia siku ya Ijumaa baada ya kula samaki huyo siku ya Jumanne ni mwanamke mmoja wa watoto wanane.

Uchunguzi wa kimaabara umethibitisha kuwa waathiriwa wote walikuwa wamekula nyama ya kasa wa baharini.

Mamlaka visiwani Zanzibar, imewataka watu  kuepuka kula kasa wa baharini.

Novemba 2021, watu saba akiwemo mtoto wa miaka mitatu walifariki dunia kisiwani Pemba baada ya kula nyama ya kasa na wengine watatu kulazwa hospitalini.

Stephen Mumbi / Dar Es Salaam/ Rfikiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.