Pata taarifa kuu

WFP inasema mapigano yanatatiza shughuli zake kwenye barabara ya Goma na Sake

Nairobi – Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, limeonya kuhusu kuendelea kwa ghasia ambazo zinatatiza shughuli zao kwenye barabara kati ya Goma na Saké, WFP ikitaka kukomeshwa kwa mapigano mashariki mwa DRC.

Mapigano kati ya jeshi la serikali ya DRC na makundi ya waasi yamekuwa yakiathiri shughuli za WFP huko Sake na Goma
Mapigano kati ya jeshi la serikali ya DRC na makundi ya waasi yamekuwa yakiathiri shughuli za WFP huko Sake na Goma AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Katika tangazo lake kupitia mtandao wa X, WFP imebainisha kuwa ghasia zinazozidi kuwa mbaya zinasababisha pengo la kibinadamu, na kulazimisha mamilioni ya watu kuishi katika hali ngumu.

Aidha Shirika hilo limesema, watu takribani laki moja ishirini na wanane waliokimbia mapigano kutoka meneo ya shasha, sake na vijiji jirani wamepewa hifadhi katika maeneo yaliyo karibu na miji ya Goma na Minova, na kwamba wengi wao hawana misaada ya kutosha.

Katika ripoti yake ya hapo jana shirika hilo la mpango wa chakula duniani WFP limesema lilisambaza tani 432 za chakula kwa zaidi ya watu 25,920 wa majanga ya asili na migogoro ya kivita huko Lushebere na Nyamukubi katika eneo la Kalehe, Kivu Kusini.

Ripoti hii inakuja wakati huu wito ukiendelea kutolewa kwa waasi wa M23 kuachana na mapigano mashariki mwa DRC, Rwanda pia ikitakiwa kuacha kuwaunga mkono waasi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.