Pata taarifa kuu

Baadhi ya raia wakosoa sanamu iliyozinduliwa kwa heshima ya Nyerere

Nairobi – Baadhi ya raia wa Tanzania, kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa sanamu mpya iliyozinduliwa kwa heshima ya rais wa zamani Julius Nyerere, wakidai haifanani naye.

Sanamu hiyo imekosolewa kwa madai kwamba haifanani na hayati Nyerere.
Sanamu hiyo imekosolewa kwa madai kwamba haifanani na hayati Nyerere. © AU
Matangazo ya kibiashara

Sanamu hiyo ilizunduliwa siku ya Jumapili, nje ya makao makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia.Viongozi kadhaa walihudhuria uzinduzi huo.

Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa taifa hilo tangu ilipojipatia uhuru wake mwaka wa 1961 hadi 1985.

Anakumbukwa kwa kupigania haki za raia wa Afrika na hata wakati mmoja kuwa mwenyeji wa baadhi ya viongozi waliokuwa wanapigania uhuru wa nchi zao, ikiwemo Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji.

Sanamu hiyo imezinduliwa jijini Addis Ababa wikendi iliopita.
Sanamu hiyo imezinduliwa jijini Addis Ababa wikendi iliopita. © Ikulu ya Tanzania

Mwaka uliopita, sanamu iliyozinduliwa kwa heshima ya rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda, iliondolewa baada ya kukashifiwa na raia kwenye taifa hilo kwamba haikuwa inafanana na Kaunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.