Pata taarifa kuu

Kenya: Rais Ruto ameendelea kukosolewa kutokana na kauli yake kuhusu Mahakama

Nairobi – Nchini Kenya, rais William Ruto ameendelea kukosolewa kwa kauli yake kuwa serikali yake haitaheshimu maamuzi ya Mahakama, yatakayopinga miradi ya serikali yake, akiwashatumu baadhi ya Majaji kuwa wafisadi na wasiojali maslahi ya umma.

Mkuu wa nchi amewashatumu baadhi ya Majaji kuwa wafisadi na wasiojali maslahi ya umma.
Mkuu wa nchi amewashatumu baadhi ya Majaji kuwa wafisadi na wasiojali maslahi ya umma. REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Jumanne ya wiki hii, rais Ruto alisema kuwa baadhi ya majaji ambao hakuwataja wanashirikiana na wanasiasa wa upinzani pamoja na watu wenye nia ya kuzuia kuendelea kwa miradi ya serikali.

Kwa upande wake Jaji mkuu kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki Martha Koome, wakati akijibu matamshi ya mkuu wa nchi alieleza kuwa kukiuka maauzi ya mahakama ni kinuyme cha sheria kwa watumishi wa umma.

Aidha Jaji Mkuu pia aliwataka Majaji wa Mhakama kuendelea na kazi yao kwa mujibu wa sheria za nchi bila ya uoga na upendeleo.

Naye Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amesema uamuzi wa Ruto ni hatari kwa demokrasia ya nchi hiyo.

“Vita hivi sio tu kuhusu Mahakama, bali ni mpango wa Ruto kuipotosha Kenya baada ya kuliteka bunge, sasa anataka kuiteka Mahakama.” alisema Odinga.

00:27

Raila Odinga kuhusu kauli ya rais Ruto dhidi ya Mahakama

Chama cha Mawakili nchini humo, nacho kimetangaza kuwa kitaandaa maandamano ya nchi nzima, kupinga kauli ya Ruto wanayosema ni kuishambulia Mahakama na Majaji.

Rais Ruto kupitia kwa taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali Hussein Mohammed siku ya Jumatano, alikiri kuendelea na vita dhidi ya kile alichokitaja kama Mahakama kutoonekana kutochukuliwa hatua.

Ruto aliyeingia madarakani mwezi Septemba mwaka wa 2022, ametuhumiwa kwa kuwaongezea raia Kenya ushuru kwa bidhaa mbalimbali haswa wakati huu wanapokabiliwa na ugumu wa maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.