Pata taarifa kuu

DR Congo: Hali imeendelea kuwa mbaya katika eneo la mashariki

Nairobi – Hali ya kibinadamu imeendelea kuwa mbaya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya masharika ya Kimataifa kutoa tadhari kwa miezi kadhaa sasa.

Uwepo wa makundi ya waasi kama M 23, umeendelea kusababisha wakaazi wa Mashariki mwa DRC kuyakimbia makwao wakihofia usalama wao
Uwepo wa makundi ya waasi kama M 23, umeendelea kusababisha wakaazi wa Mashariki mwa DRC kuyakimbia makwao wakihofia usalama wao AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

Uwepo wa makundi ya waasi kama M 23, umeendelea kusababisha wakaazi wa Mashariki mwa DRC kuyakimbia makwao wakihofia usalama wao, na sasa wanaishi kwenye mazingira magumu.

Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP linasema watu zaidi ya Milioni tatu wanaoishi kwenye kambi mbalimbali mkoani Ituri, Kivu Kaskazini na Kusini, wanahitaji msaada wa haraka kama chakula na dawa.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa DRC haipokei msaada wa kutosha kuwasaidia raia waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya utovu wa usalama
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa DRC haipokei msaada wa kutosha kuwasaidia raia waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya utovu wa usalama AFP - GUERCHOM NDEBO

Aidha, wakimbizi hao wa ndani wanaoshi kwenye mazingira magumu hasa kipindi cha mvua. Hakuna mahema ya kutosha na mkusanyiko mkubwa wa watu unaelezwa kuwa tishio kwa hali yao ya kiafya kwa sababu kuna wasiwasi wa kutokea kwa mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.

Kuwasaidia watu hao, zaidi ya Dola Milioni 630 zinahitajika. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa DRC haipokei msaada wa kutosha kuwasaidia raia waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya utovu wa usalama, na mwaka huu ni asilimia 20 tu ya msaada wa fedha ndio uliopatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.