Kenya: Odinga asema hatozungumza na Ruto bila mpatanishi
Nchini Kenya, kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema hatazungumza na rais William Ruto bila ya kuwepo kwa mpatanishi kwa kile anaeleza kuwa kiongozi huyo haaminiki.
Imechapishwa:
Msimamo huu wa Odinga unakuja baada ya Ruto kusema kuwa, yupo tayari kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mpinzani wake baada ya kushuhudiwa maandamano ya wiki kadhaa, kupinga kupanda kwa gharama ya maisha, miongoni mwa mambo mengine, yaliyosababisha maafa na majeruhi ya waandamanaji.
Odinga alisitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchi nzima na kuwataka wafuasi wake kutumia wiki hii kuwaomboleza watu waliopoteza maisha wakati huu akipanga kulishtaki jeshi la polisi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa kuwaua waandamanaji.
Lakini je? Kuna utashi wa kisiasa katika hili? Dokta Bryan wanyama ni mtaalamu wa siasa za Kenya na mhadhiri katika chuo kikuu cha kibabii kilichopo Bungoma.
‘‘Cha msingi hapa Kenya ni yetu sisi sote na wakati kama huu ni muhimu wakati ndugu wawili wanapokuwa na matatizo wakae pamoja kutafuta suluhu.” alisma Dokta Bryan wanyama.
Dokta Bryan wanyama ni mtaalamu wa siasa
Muungano wa upinzani unalaumu ukatili wa polisi kwa vifo hivyo, lakini wizara ya mambo ya ndani imetetea hatua iliyochukuliwa na maofisa wa usalama kuwakabili waandamanaji.
Mapema siku hiyo, viongozi wa upinzani, akiwemo Odinga, walizuru hospitali mbalimbali jijini Nairobi kuwatembelea watu waliojeruhiwa wakati wa maandamano hayo.
As we visited and condoled with the victims of police brutality today at Mama Lucy and Kenyatta National hospitals respectively, the words from the Book of Isaiah 1:17 that we should "Learn to do good; seek justice, correct oppression; bring justice to the fatherless, and plead… pic.twitter.com/VW9wochoeE
— Kalonzo Musyoka (@skmusyoka) July 26, 2023
Mwanasiasa wa upinzani Kalonzo Musyoka alisema ni muhimu haki ipatikane kwa ajili yao.Tangazo kuhusu maandamano zaidi litatolewa Ijumaa, alisema.
Wanadiplomasia na makundi ya kutetea haki za binadamu wameitaka serikali na upinzani kutatua tofauti zao kwa amani.