Pata taarifa kuu

DRC yakaribisha ripoti ya UN kuhusu Rwanda na M23

NAIROBI – Serikali ya DRC imekaribisha ripoti ya Kundi la wataalamu wa umoja wa mataifa, ambapo wanadai kuwa wamekusanya taarifa za ziada kuhusika kwa jeshi la Rwanda na waasi wa M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini kutekeleza mauaji, ubakaji na ukiukaji wa haki za binadamu, licha ya Rwanda kukanusha.

Rwanda imekuwa ikituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23
Rwanda imekuwa ikituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Kundi la waasi ADF lilishambulia shule moja eneo la Kasese,Uganda na kuwauwa watu zaidi ya 40,limeendelea kupanua shughuli zake katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,likifadhiliwa na kundi la kijihadi la Islamic State,wamesema watalaam wa umoja wa mataifa.

Patrick Muyaya ni msemaji wa serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

“Kabla ya ripoti hii kutolewa, wanadiplomasia kutoka DRC wamekuwa na taarfia hiyo kwa sababu wanazozana zote, hakuna jambo linalofanyika eneo la mashariki bila ya kuonekana kupitia ndege zao zisizo na rubani.” alisema Patrick Muyaya.

00:41

Patrick Muyayani, msemaji wa serikali ya DRC

Aidha amesema kuwa ripoti peke yake haitoshi na kwamba vikwazo vinahitajika kutolewa pamoja na hukumu kwa kuzingatia sheria.

Haya yanajrii wakati huu mashirika ya misaada ya umoja wa Mataifa, yakitoa wito wa dharura kuwasaidia mamilioni ya raia nchini DRC, ambako kunashuhudiwa muendelezo wa machafuko yaliyosababisha maelfu ya raia kukimbia.

Kwa mujibu wa shirika la WFP, tangu machi mwaka jana, watu zaidi ya milioni 5 walikimbia. Tomson Phiri, ni msemaji wa shirika hilo ukanda wa kusini mwa Afrika.

“Nchini DRC, kama baadhi yenu mnavyofahamu, ni nchi yenye masuala mtambuka, nchi ambayo inazalisha vitu vyenye thamani vinavyotumika kwenye tekenolojia ya kisasa lakini ndio nchi ambayo inakabiliwa na usalama mdogo wa chakula duniani.” alieleza Tomson Phiri, msemaji wa WFP.

00:35

Tomson Phiri, ni msemaji wa WFP

Makundi ya waasi yameripotiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia katika eneo la Mashariki ya DRC ambapo mamilioni ya raia wametoroka wikihofia kushambuliwa.

Licha ya wito kuendelea kutolewa na jamii ya kimataifa kwa Makundi yenye silaha Katika eneo hilo kuachana na mapigano, wito huo umeonekana kutoheshimiwa.

Waasi wamendelea kutekeleza mashambulio licha ya uwepo wa vikosi vya walinda usalama kutoka mataifa ya ukanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.