Pata taarifa kuu

Rwanda yatuhumiwa kutoa taarifa za uongo kwa Interpol kuhusu wapinzani walio uhamishoni

Mamlaka ya Rwanda yanahusishwa katika uchunguzi uliochapishwa na muungano wa wanahabari, Organized Crime and Corruption Reporting Project (OCCRP). Ili kuwashtaki wapinzani wa kisiasa nje ya nchi, Rwanda inadaiwa kutoa taarifa za uongo za kijasusi kwa Marekani na Interpol. OCCRP inaonyesha hasa maudhui ya ripoti ya FBI kuhusu suala hili.

Eugène-Richard Gasana, balozi wa zamani wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa na sasa ni mpinzani wa Kigali.
Eugène-Richard Gasana, balozi wa zamani wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa na sasa ni mpinzani wa Kigali. © STAN HONDA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waraka huo uliotolewa mwaka wa 2015, unasema mamlaka ya utekelezaji wa sheria ya Marekani kwa muda mrefu imekuwa ikifahamu mbinu zinazotumiwa na Kigali kupambana na raia wa Rwanda waishio katika ardhi ya Marekani.

Katika ripoti hii, FBI inawatahadharisha wanadiplomasia wa juu zaidi wa Marekani kuhusu mbinu zinazotumiwa na idara ya kijasusi ya Rwanda kuhadaa mamlaka kuhusu waomba hifadhi na wapinzani wa Rwanda. Njia yao ya kufanya kazi ni "kutoa taarifa za uongo au za kupotosha kimakusudi kwa vyombo vya kutekeleza sheria kuhusu madai ya makosa ya jinai kwa msaada wa maafisa wa taasisi hii, pamoja na kujaribu kutumia vibaya sheria ya uhamiaji."

Wapinzani kadhaa wameripotiwa kulengwa, wakiwemo watu wenye mfungamano na vuguvugu la Rwanda National Congress (RNC), vuguvugu linalompinga Rais Paul Kagame. FBI inasema iliwachunguza watu hawa, lakini haikupata ushahidi wa vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, ripoti hii inahakikisha, uchunguzi huu "ulitatizwa kimfumo" na idara ya kijasusi ya Rwanda.

Shirika la Marekani pia linaishutumu serikali ya Rwanda kwa kujaribu kuendesha Interpol na mfumo wake wa notisi nyekundu. Katika uchunguzi wake, muungano wa wanahabari unafichua kwamba hivi karibuni Interpol ilibatilisha hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi ya Eugène-Richard Gasana, mfuasi wa zamani wa Paul Kagame, ambaye sasa hana ushirikiano wowote na utawala. Hati ya kukamatwa ilibatilishwa kwa sababu ya "mwelekeo mkubwa wa kisiasa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.