Pata taarifa kuu
TANZANIA-AFYA

Tanzania yatangaza masharti mapya kudhibiti kusambaa kwa COVID-19

Wizara ya afya nchini Tanzania, imetangaza masharti mapya yanayolenga kusaidia kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Wiki iliyopita, Tanzania ilipokea dozi zaidi ya Milioni moja ya chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Marekani kupitia mfumo wa Covax.
Wiki iliyopita, Tanzania ilipokea dozi zaidi ya Milioni moja ya chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Marekani kupitia mfumo wa Covax. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watu nchini humo wametakiwa kuvaa barakoa kila wakati na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, ikiwa ni pamoja na wito wa kuahirishwa kwa sherehe za harusi, huku mikusanyiko ya watu kwenye majumba ya Ibada ikitakiwa kupungua.

Wiki iliyopita, Tanzania ilipokea dozi zaidi ya Milioni moja ya chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Marekani kupitia mfumo wa Covax.

Marekani imesema kwamba hatua hiyo ni miongoni mwa mpango wa kusambaza dozi milioni 25 za chanjo katika mataifa ya Afrika.

Chanjo hizo zitatumika na mahujaji, wafanyakazi wa afya, wale wa huduma za hoteli, wafanyakazi wa balozi na wagonjwa wa corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.