Pata taarifa kuu

G7 yatangaza bei ya dola 60 kwa pipa ya mafuta ya Urusi

Lengo ni kuinyima Moscow uwezo wa kufadhili vita nchini Ukraine. Urusi imepata euro bilioni 67 kutokana na mauzo yake ya mafuta kwa Umoja wa Ulaya (EU) tangu kuanza kwa vita hivyo.

Kiwanda cha kuzalisha dizeli katika eneo la mtambo wa Yarakta, kinachomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Irkutsk (INK), katika jimbo la Irkutsk, Urusi.
Kiwanda cha kuzalisha dizeli katika eneo la mtambo wa Yarakta, kinachomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Irkutsk (INK), katika jimbo la Irkutsk, Urusi. © REUTERS/Vasily Fedosenko VASILY FEDOSENKO
Matangazo ya kibiashara

Bei ya mafuta inayouzwa na Urusi kwa nchi za Magharibi itafikia dola 60 kwa pipa kuanzia siku chache zijazo, nchi za Umoja wa Ulaya, kisha zile za kundi la nchi zilizotsawi kiuchumi (G7) na Australia zilifikia makubaliano siku ya Ijumaa siku tatu kabla ya kuanza kutekelezwa kwa vikwazo vya Ulaya.

"G7 na Australia (...) zimefikia makubaliano juu ya bei ya juu ya dola 60 za Kimarekani kwa pipa kwa mafuta ghafi ya asili ya Urusi yanayosafirishwa kwa bahari", zilitangaza nchi hizi katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amekaribisha tangazo hilo katika taarifa yake, ambayo "ni kilele cha miezi ya juhudi za muungano wetu".

Makubaliano hayo yalifanikishwa na maafikiano yaliyofikiwa mapema leo na nchi 27 za Umoja wa Ulaya, ambazo zimefaulu kuiunganisha Poland.

Mawaziri wa fedha wa nchi za G7 walikubaliana mapema mwezi Septemba juu ya chombo hiki, kilichoundwa kuinyima Moscow uwezo wa kufadhili vita vyake nchini Ukraine.

Kwa maneno madhubuti, bei iliyowekwa lazima iwe ya juu vya kutosha kwa Urusi kuwa na nia ya kuendelea kuwauzia mafuta, lakini chini ya bei ili kupunguza mapato ambayo inaweza kupata kutoka kwake.

Utaratibu huo utaanza kutumika Jumatatu "au hivi karibuni", imebainisha G7 na Australia. Hakika ni Jumatatu ambapo vikwazo vya EU vinaanza kwa mafuta ya Urusi yanayosafirishwa kwa bahari.

Kwa hivyo, mafuta pekee yanayouzwa na Urusi kwa bei sawa au chini ya dola 60 yanaweza kuendelea kutolewa. Zaidi ya dola 60, itakuwa marufuku kwa makampuni kutoa huduma zinazowezesha usafiri wa baharini (mizigo, bima, nk).

Hivi sasa, nchi za G7 zinatoa huduma za bima kwa 90% ya shehena ya kimataifa na EU ni mdau mkuu katika usafirishaji wa mizigo baharini - kutoa kizuizi cha kuaminika, lakini pia hatari ya kupoteza masoko kwa washindani.

Marekebisho ya bei

Urusi, nchi ya pili duniani kwa uuzaji nje wa bidhaa ghafi, kwa upande wake ilionya kwamba haitapeleka tena mafuta kwa nchi ambazo zitaidhinisha kiwango hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.