Pata taarifa kuu

Urusi yaendelea kulenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine

Vituo vitatu vipya vya umeme viliharibiwa Jumatano Oktoba 19, kulingana na mamlaka ya Ukraine ambayo inawaomba raia wa Ukraine kupunguza matumizi yao ya umeme.

Katika mtaa wa Zaporizhia, Ukraine, Jumatano, Oktoba 19, 2022.
Katika mtaa wa Zaporizhia, Ukraine, Jumatano, Oktoba 19, 2022. AP - Leo Correa
Matangazo ya kibiashara

Katika mikoa yote ya nchi, matumizi ya umeme yamepunguzwa kati ya saa moja asubuhi na tano usiku. Vinginevyo raia wa Ukraine wanatakiwa kujiandaa kwa kukatika kwa umeme kila mara. Hii ina maana kwamba watu binafsi vitu vinavyotumia umeme mwingi kama vile viyoyozi, hita za umeme. Na katika makampuni, maduka na migahawa, itakuwa muhimu kupunguza mwanga wa ishara, skrini na nafasi za matangazo.

Serikali inajadili mambo kadhaa yanayowezekana. Ikiwa ni pamoja na hali mbaya zaidi: uharibifu au uondoaji wa mitambo yote ya umeme ya Ukraine.

Hadi sasa, 30% hadi 40% ya mitambo ya umeme imelengwa. Mamlaka inatafuta suluhu za dharura kama vile kuunda vituo vya usambazaji wa umeme katika miji na vijiji ili kudumisha shughuli za miundombinu nyeti zaidi. Kazi hiyo inaonekana kuwa ngumu kwa Ukrenergo, shirika la umeme ambalo makao yake makuu yalilengwa siku chache zilizopita katikati mwa mji wa Kyiv na shambulio la ndege isiyo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.