Zaidi ya watu 33,000 raia wa Gaza wameuawa katika miezi 6 iliyopita
Takwimu ambazo zimerekodiwa tangu vita vilivyozuka zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 33,000 kutoka Gaza, wengi wao wakiwa raia, wameuawa, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina inayoendeshwa na Hamas.
Imechapishwa:
Utafiti wa hivi karibuni uliyofanya Aprili 5 unaonyesha kuwa zaidi ya 70% ya waliouawa walikuwa wanawake na watoto.
Kwa mujibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Save the Children, watoto 13,800 wa Kipalestina huko Gaza wameuawa na zaidi ya 12,009 kujeruhiwa. Unicef inaripoti kuwa angalau watoto 1,000 wamekatwa mguu mmoja au miguu yote miwili.
Zaidi ya watu milioni 1.7 wamekimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.