Pata taarifa kuu

Gaza: Israel yashambulia Gaza wakati wa sikukuu ya Eid licha ya kukemewa na Marekani

Israeli imeshambulia eneo la Gaza leo, wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha sherehe za Eid za kutamatika mfungo wa Ramadhan, shambulio linalojiri hata baada ya Marekani Kuonya Israel kuhusu mpango wake katika vita hivyo.

Eneo la shambulizi la anga la Israel kwenye jengo, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la waislamu wa Palestina Hamas, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. April 2, 20
Eneo la shambulizi la anga la Israel kwenye jengo, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la waislamu wa Palestina Hamas, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. REUTERS - Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya  Wapelestina  waliojumuika kusherekea EID katika sehemu tofauti ikiwemo msikitu mkubwa wa Al-Aqsa,walielezea masikitiko yao kuwa walilazimika kusali  wakati makazi yao yakiwa ni  vifusi .

Walielezea tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikusanyika katika msikiti huo, kusherekea ,walikutanyika, kutia moyo .

Israel imefanya mashambulio hayo ya ardhini na anga, siku moja baada ya waziri mkuu Benjamini Netanyahu kuapa kuwamaliza wapiganaji wa Hamas na kuwarudisha nyumbani mateka wa Israel.

Shambulio hili pia limetokea wakati mazungumzo ya Cairo kujaribu kutatuta mwafaka yakiongozwa na Misri, Qatar na  Marekani, rais Biden akiwa amemwonya Netanyahu kuendelea kufanya kosa katika mbinu anazotumia katika mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.