Pata taarifa kuu
Sudani-mapigano

Pande zinazohasimiana zaendelea kukwamisha misaada kufika Sudan Kusini

Pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini zimezuia misaada ya kibinadamu kuwafikia maelfu ya raia ambao waliyakimbia makazi yao tangu miezi mitatu iliyopita kufuatia mzozo huo,afisa moja wa Umoja wa mataifa amearifu.

Waasi wa Darfur nchini Sudan Kusini
Waasi wa Darfur nchini Sudan Kusini
Matangazo ya kibiashara

Takribani magari 50 yaliyobeba misaada mbalimbali ikiwemo vyakula na madawa yamekwama kuingia katika taifa hilo lenye makabiliano huku waasi na serikali wakichelewesha misaada hiyo kuingia.

Hali imekuwa ngumu kwa wafanyakazi wa misaada waliopo katika maeneo ya mapigano huko sudan ambapo jana Mfanyakazi mmoja wa shirika la kimataifa la msalaba mwenkundi la CICR ameuwa jijini Darfour wakati huu vurugu zikiendelea kuripotiwa huko magharibi mwa Sudani.

Najmaddin Salih Musa Bishara, ambaye alikuwa anafanya kazi katika ghala la shirika hilo la msalaba mwekundu aliuawa kwa kupigwa risasi.

Katika taarifa iliotolewa na shirika hilo haikuweka wazi kuhusu hatma ya wafanyakazi wengine waliokuwemo katika gari la shirika hilo. Tangu Februari Mosi mwaka huu serikali ya Kharthoum ilisitisha shughuli za shirika hilo la kimataifa la msalaba mwekundu CICR ikilituhumu kuvuka mpaka katika kutekeleza shughuli zake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.