Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Diplomasia

Hali imekua nzito katika kisiwa cha Crimea

Baada ya matokeo ya kura ya maoni katika kisiwa cha Crimea,rais wa Urusi Vladmir Putinametia sainikwenye mkataba wa kunganisha kisiwa hicho na Urusi. Huku tuhuma za kulani zikiendelea kuongezeka kutoka kwa Marekani na Umoja wa Ulaya, idadi ya wanajeshi imekua ikiongezwa karibu na kisiwa hicho.

Wanajeshi wa Ukraine karibu ya kijiji cha Salkovo katika eneo la Crimea, machi 18 mwaka 2014.
Wanajeshi wa Ukraine karibu ya kijiji cha Salkovo katika eneo la Crimea, machi 18 mwaka 2014. REUTERS/Viktor Gurniak
Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi mmoja wa Ukraine ameuawa jana katika kisiwa cha Cimea. Wakati huohuo waziri wa ulinzi wa Ukraine amewamuru wanajeshi wa Ukraine walioko katika kisiwa cha Crimea kutumia silaha zao.

Hakuna damu ambayo ilikua imesha mwagika hadi muda huu. Lakini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa ulinzi wa Ukraine, wanajeshi wa Urusi wamempiga risase jana mwanajeshi mmoja wa Ukraine.

Mwanajeshi huyo ameuawa wakati wa mashambulizi dhidi ya kikosi cha wanajeshi wa Ukraine walipovamiwa katika mji wa Simferopol, taarifa hii ni kwa mujibu wa jeshi mjini Kiev. Punde tu baada ya taarifa ya kifo cha afisa wa jeshi, waziri mkuu wa Ukraine, Arseni Iatseniouk, amelani kitendo hicho na kubaini kwamba ni “uhalifu wa kivita”.

Ameongeza kusema pia kwamba, mzozo huo umetoka “hatua ya kisiasa na kuingia katika hatua ya kijeshi”. Wakati huohuo, serikali ya Ukraine imeamuru wanajeshi wake kutumia silaha zao ikihitajika, ili kulinda usalama wao.

Tangu jumapili machi 16, hali ya mambo imeendelea kubadili taswira. Baada ya matokeo ya kura ya maoni 17 machi, ambapo raia wa Crimea walipiga kura ya kujiunga na Urusi kwa asilimia 96. Na tangu jumatatu, bunge la Crimea lilitangaza kwamba Crimea imejitenga na Urusi na kuomba rasmi kujiunga na Urusi.

Baadae jioni, rais wa Urusi Vladmir Putin alitia saini ya kutambua uhuru wa Crimea , na jumanne 18 machi mchana, sheria ya kujiunga kwa Cimea na Urusi ikasainiwa na mataifa hayo mawili. Bunge la Moscow linasubiriwa kuidhinisha sheria ya kujiunga kwa mataifa ya Crimea na Urusi.

Umoja wa Ulaya umesema hautambui wala hautotambua kujiunga kwa Crimea na Urusi. Katika miji ya Ulaya kauli ni hio.

“Ni masikitiko makubwa kuona Urusi unakubali uamzi wa Cimea wa kujitenga na Ukraine”, amesema William Hague, Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uingereza, amesema nchi yake itasitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Moscow.

Ujerumani kupitia, waziri mkuu wa nchi hio, kanzsela Angela Merkel, amependekeza kuanzishwa kwa mazungumzo mapya, huku akilani mkataba “dhidi ya haki ya kimataifa”.

Kwa upande wake rais wa Ufaransa, François Hollande, kikao Umoja wa Ulaya cha hivi karibunikitakachofanyika tarehe 20 na 21 machi kitatoa fursa kwa uamzi mkali utakaochukuliwa kufuatia msimamo wa Urusi wa kukubali kujiunga na Crimea.

Rais wa Marekani Barack Obama, amependekeza mkutano wa viongozi wamatifa 7 yaliyoendelea kiviwanda (G7) na Umoja wa Mataifa mjini La Haye ili kujadili hali inayojiri nchini Ukraine.

Kikao hiki, ni namna nyingine, kama inahitajika, kuonesha Urusi kwamba imekua ikijitenga kila mara peke yake katika mataifa yaliendelea kiviwanda, amesema Obama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.