Watu 70 wauwawa nchini Syria siku chache kabla ya ziara ya Kofi Annan nchini humo
Zaidi ya watu 70 wameuwawa nchini Syria jana Ijumaa,wakati makumi ya maelfu ya waandamanaji wakiandamana mitaani huku mizinga ikitumika kuwatawanya waandamanaji katika mji wa Damascus, waangalizi nchini humo wamesema.
Imechapishwa:
Machafuko hayo mapya yametokea wakati mjumbe wa umoja wa mataifa na jumuiya ya nchi za Kiarabu Kofi Annan ambaye anaongoza mpango wa kusitisha mapigano nchini humo akikamilisha mpango wa kurejea Damascus.
Wanadiplomasia mjini Geneva wamesema kuwa katibu mkuu huyo wa zamani wa Umoja wa mataifa anataraji kuzuru mji mkuu wa Syria mapema wiki ijayo.
Kofi Annan amekuwa akiongoza mpango wa kumaliza machafuko na umwagaji damu nchini Syria, mpango ambao hata hivyo umekuwa ukivunjwa mara kadhaa.