Pata taarifa kuu

Marekani na China zakubaliana kufanya mazungumzo kuhusu ukuaji wa uchumi wenye uwiano

Marekani na China zimekubali kuwa na "majadiliano ya kina juu ya ukuaji wa uwiano", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Idara ya Fedha ya Marekani iliyochapishwa siku ya Jumamosi Aprili 6, kufuatia mazungumzo ya siku mili kati ya Waziri wa Mambo ya Nje, Janet Yellen, na mwenzake wa China, He Lifeng, huko Guangzhou (Canton). Waziri wa Fedha wa Marekani pia ameonya makampuni ya China ambayo yatatoa msaada kwa Urusi.

Janet Yellen, Aprili 6, 2024 huko Guangzhou (Canton).
Janet Yellen, Aprili 6, 2024 huko Guangzhou (Canton). AFP - PEDRO PARDO
Matangazo ya kibiashara

"Mazungumzo haya yajayo kati ya Marekani na China yanaonesha jaribio jipya la kuleta utulivu wa mahusiano kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani tangu mkutano kati ya Marais Joe Biden na Xi Jinping mwezi Novemba 2023. "Yatawezesha mjadala kuhusu kukosekana kwa usawa wa uchumi mkuu na ninakusudia kuchukua fursa hii kutetea usawa kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa Marekani,” Yellen amesema katika taarifa tofauti.

Tahadhari

Ziara ya Bi. Yellen, ambayo ni ya pili kwa China katika mwaka mmoja, inakuja wakati Washington na Beijing hazikubaliani juu ya masuala kadhaa, kama vile ufikiaji wa teknolojia ya hali ya juu, mustakabali wa Taiwan au programu ya video ya TikTok. Waziri wa Fedha wa Marekani pia ameonya makampuni ya China ambayo yatatoa msaada kwa Urusi na sekta yake ya ulinzi katika vita vya Ukraine.

Bi Yellen amesisitiza kwamba "kampuni, haswa za China, hazipaswi kutoa msaada wa vifaa kwa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, kwa tasnia ya ulinzi ya Urusi" na kutishia "athari kubwa" kwa wale waltakaofanya hivyo, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Ruzuku kwa viwanda, "hatari"

Janet Yellen aliwasili China mnamo Aprili 4 kwa zaiara ya siku nne, na kituo cha kwanza ilikuwa huko Canton (Guangzhou), kisha alitarajia kwenda Beijing siku ya Jumamosi Aprili 6. Jana, Ijumaa, Waziri wa Fedha wa Marekani alithibitisha kuwa ruzuku iliyolipwa na Beijing kwa sekta hiyo iliwakilisha "hatari kwa ustahimilivu wa kiuchumi wa kimataifa", kwa kuunda "uwezo mkubwa" wa uzalishaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.