Pata taarifa kuu

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen azuru China katika hali ya mvutano

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili China tarehe 4 Aprili kwa mara ya pili katika muda wa chini ya mwaka mmoja. Huko Guangzhou kusini mwa nchi, atakutana na wakuu wa makampuni, raia wa Marekani na Makamu wa Waziri Mkuu He Lifeng. Lakini zaidi ya ziara yake itafanyika Beijing. Janet Yellen anatarajiwa kukutana na mwenzake Lan Fo'an, Waziri Mkuu Li Qiang na Gavana wa Benki Kuu Pan Gongsheng.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou Baiyun huko Guangzhou, jimbo la Guangdong, China Aprili 4, 2024.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou Baiyun huko Guangzhou, jimbo la Guangdong, China Aprili 4, 2024. REUTERS - Tingshu Wang
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa zimeboresha zaidi uhisiano wao katika miezi ya hivi karibuni, lakini Waziri wa Fedha wa Marekani atafanya kinachowezekana ili kupunguza mvutano ambao bado uko juu.

Machoni mwa Beijing, Janet Yellen hayumo katika orodha ya vigogo wa Marekani walio na chuki na China na kwa hivyo wenzake wana imani naye. Lakini je, ataweza kuishawishi China kuacha kupiku soko la kimataifa kwa magari yake ya bei ya chini ya umeme, betri na paneli za jua, kitendo ambacho Washington inaona kuwa "sio ya haki"? Hakuna uhakika.

Usalama wa taifa wa Marekani mashakani

Kudorora kwa uchumi wake kunaisukuma China kudumisha uzalishaji wake kupita kiasi. Lakini Washington inahofia kwamba matukio ynayoitikisa China hivi sasa yataathiri uchumi wa dunia na kuahidi kutokaa kimya. Hata kama hali sio nzuri na Beijing ilitaja mazungumzo ya Jumanne Aprili 2 kati ya Rais Biden wa Marekani na mwenzake wa China Xi Jinping kuwa "ya kweli na ya kina," maswala yanayoghadhabisha hayakosi.

Washington inafikiria kupiga marufuku uwekezaji fulani wa Marekani nchini China kwa sababu za usalama wa taifa, hii inahusu hasa magari madogo, magari haya ya kielektroniki ambayo China inahitaji sana ikiwa inataka kuboresha uchumi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.