Pata taarifa kuu

Puto nane za China zaruka juu ya anga ya Taiwan siku mbili mfululizo

Chokochoko za China zinaendelea kuzunguka Taiwan na zinachukua sura mpya: Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imedai siku ya Jumapili kuwa imegundua puto nane za China zikizunguka Taiwan kwa siku ya pili mfululizo, wikendi wakati pande zote za mlango wa bahari, zinaadhimisha Mwaka Mpya wa Mwezi. Beijing inakichukulia kisiwa cha Taiwan kama sehemu ya ardhi yake na haijawahi kukataa kutumia nguvu ili kupata udhibiti tena.

Puto nyeupe karibu na bendera ya China wakati wa maandamano mbele ya ubalozi wa China nchini Marekani, Februari 15, 2023.
Puto nyeupe karibu na bendera ya China wakati wa maandamano mbele ya ubalozi wa China nchini Marekani, Februari 15, 2023. AFP - SAUL LOEB
Matangazo ya kibiashara

 

Puto tano kati ya nane ziliruka moja kwa moja juu ya anga yaTaiwan kutoka mashariki hadi magharibi, la sita lilielekea ncha ya kaskazini ya kisiwa, kama inavyoonyeshwa kwenye ramani iliyochapishwa na Wizara ya Ulinzi. Puto zote zilionekana Jumamosi, Mwaka Mpya wa Lunar ukiadhimishwa pande zote mbili za Mlango wa Bahari wa Taiwan, katika mwinuko kati ya 3,600 na 10,700 m, kulingana na chanzo hicho. Tayari siku iliyotangulia, wizara ilitangaza idadi kubwa ya puto. Mnamo Februari 2023, jeshi la Taiwan lilitoa taarifa kwa mamlaka ya usafiri wa anga baada ya kugundua puto ikiruka juu ya anga ya Taiwan, lakini halikutaarifu kuhusu asili ya puto hiloau mahali lilipo.

Chokochoko za China

Kwa hakika Beijing sio chokochoko wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, jeshi pia lilirusha hewani video kama nia njema, likionyesha meli za kivita na ndege za kivita karibu na Taiwan, huku nyuma kuna wimbo wa kusifu kuungana tena na bara la China. Na tarehe 30 Januari, China ilichukua uhuru wa kubadilisha njia yake ya anga ya ndege yenye chapa M503 bila kwanza kushauriana na mamlaka ya Taiwan. Ndege za kibiashara za China sasa zitapita karibu na pwani ya Taiwan, hali ambayo inatia wasiwasi Taipei.

Chokochoko hizo zinakuja wakati Lai Ching-te wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo alishinda uchaguzi wa rais mwezi mmoja tu uliopita - "mtengano hatari" machoni pa Beijing ambayo ilikuwa imeonya kwamba ushindi wa Lai ungesababisha Taiwan kuingia "vitani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.