Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Washington yaidhinisha kutuma silaha Taiwan kama sehemu ya mpango wa msaada wa kijeshi

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden umeidhinisha msaada wa moja kwa moja wa kijeshi kwa Taiwan, kwa mara ya kwanza kama sehemu ya mfuko wa msaada kwa serikali za kigeni, maafisa walisema siku ya Jumatano.

Makao makuu ya Baraza la Bunge na Bunge la Seneti, huko Washington.
Makao makuu ya Baraza la Bunge na Bunge la Seneti, huko Washington. AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje iliarifu Bunge siku ya Jumanne kuhusu kuipta Taiwan msaada wa dola milioni 80 (euro milioni 73), kiasi kidogo ikilinganishwa na mauzo yake ya hivi majuzi ya silaha kwa Taiwan, lakini ambayo itakuwa ya kwanza kwa Taipei chini ya Mpango wa Ufadhili wa Kijeshi wa Ng'ambo.

Tangazo hili kwa vyovyote vile litaikasiriha Beijing. Tawala za Marekani zilizofuatana zimefanya hivi kupitia mauzo badala ya misaada ya moja kwa moja kwa Taiwan.

'Amani na utulivu wa kikanda'

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesisitiza kuwa msaada huu wa kwanza kabisa unaotolewa chini ya mpango huu haumaanishi kutambuliwa kwa uhuru wa Taiwan. "Kulingana na Sheria ya Mahusiano ya Taiwan na sera yetu ya muda mrefu ya China Moja, ambayo haijabadilika, Marekani inaipatia Taiwan ulinzi wa bidhaa na huduma unaohitajika ili kuiwezesha kudumisha uwezo wa kutosha wa kujilinda," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani amesema.

"Marekani ina nia ya kuendelea katika (kudumisha) amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan, ambao ni muhimu kwa usalama na ustawi wa kikanda na kimataifa," amesema. Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imetoa shukrani zake. "Msaada huu utachangia amani na utulivu wa kikanda," imesema katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari. Wizara ya Mambo ya Nje haijatangaza rasmi msaada huo au kutoa maelezo. 

Wabunge wwote kutoka vyama vya Democratic na Republican wanaunga mkono mpango wa kuipa silha Taiwan. 

Katika miezi ya hivi karibuni, Beijing na Washington zimeanzisha upya mazungumzo na mfululizo wa ziara za maafisa wakuu wa Marekani huko Beijing, ikiwa ni pamoja na mkuu wa diplomasia Antony Blinken. Lakini Taiwan bado ni kikwazo, huku mamlaka za China zikiongeza maonyo na kuona Marekani ikiwa na nia ya kuunga mkono uhuru rasmi wa kisiwa hicho. Katika muda wa mwaka mmoja tu, Beijing imefanya mazoezi makubwa ya kijeshi mara tatu kujibu ziara za viongozi wa Taiwan au Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.