Pata taarifa kuu

Taiwan yanasa ndege 103 za kivita za China kwenye anaga yake

Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema leo Jumatatu kuwa imenasa ndege 103 za kivita za China karibu na kisiwa hicho katika muda wa saa 24, idadi kubwa isiyo kawaida.

Luteka ya kijeshi mnamo Mei 30, 2019 huko Taiwan.
Luteka ya kijeshi mnamo Mei 30, 2019 huko Taiwan. © SAM YEH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kati ya Septemba 17 na 18 asubuhi, Wizara ya Ulinzi imenasa jumla ya ndege 103 za China, ikiwa ni rekodi katika kipindi cha hivi karibuni na inaleta matatizo makubwa ya usalama katika pande zote za mlango wa bahari wa Taiwan na katika kanda," wizara imesema katika taarifa yake.

"Uchochezi wa kijeshi unaoendelea" kutoka Uchina "unaweza kusababisha kuongezeka kwa mvutano na kuzorota kwa usalama katika eneo hilo," imeonya wizara hiyo, ambayo inaitaka Beijing "kukomesha mara moja vitendo hivi vya uharibifu vya upande mmoja."

Kati ya idadi ya ndege za kijeshi zilizonaswa, 40 zilivuka mstari wa wastani - mpaka usio rasmi kati ya China na Taiwan ambao China haitambui - na kuingia katika zili katika eneo la utambulisho wa ulinzi wa anga wa kusini (Adiz) -magharibi na kusini mashariki, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari. Meli tisa za kivita za China pia zilionekana karibu na kisiwa hicho.

Mazoezi kadhaa ya kijeshi katika miezi ya hivi karibuni

Adiz, inajumuisha eneo pana zaidi ambalo ndege yoyote ya kigeni inapaswa kujitangaza kwa mamlaka za anga za ndani. Adiz ya Taiwan inaingiliana na sehemu ya ile ya China na hata inajumuisha sehemu ya bara.

Serikali ya China inakichukulia kisiwa hicho kinachojitawala kama sehemu ya eneo lake ambalo imeapa siku moja kuungana tena, kwa nguvu ikiwa ni lazima. Beijing imezidisha vitisho vyake na shinikizo la kisiasa na kiuchumi kwa Taiwan tangu rais Tsai Ing-wen aingie madarakani mwaka 2016, kutoka kwa chama kinachotetea tangazo rasmi la uhuru wa kisiwa hicho.

Mwezi Aprili mwaka huu, Beijing ilifanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho, baada ya mkutano kati ya rais wa Taiwan na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy huko California.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.