Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Taiwan: Mgombea asieyependwa na China, Lai Ching-te, ashinda uchaguzi wa rais

Lai Ching-te, mgombea katika uchaguzi wa urais wa Taiwan uliowasilishwa na China kama "hatari kubwa", kwa mujibu wa karibu matokeo rasmi ya mwisho, ameshinda kura; Hou Yu-ih, mgombea anayeunga mkono uhusiano na Beijing amekubali kushindwa. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Umoja wa Ulaya "unawapongeza wapiga kura wote" walioshiriki katika "zoezi hili la kidemokrasia".

Wafuasi wa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Lai Ching-te wakishangilia matokeo ya uchaguzi huko Taipei, Taiwan, Januari 13, 2024.
Wafuasi wa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Lai Ching-te wakishangilia matokeo ya uchaguzi huko Taipei, Taiwan, Januari 13, 2024. © AP/ChiangYing-ying
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Taiwan, Kuomintang (KMT), ambacho kinaunga mkono uhusiano na China, amekubali kushindwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi Januari 13 jioni. “Ninaheshimu uamuzi wa mwisho wa raia wa Taiwan” na “Nawapongeza Lai Ching-te na Hsiao Bi-khim (mgombea mwenza) kwa kuchaguliwa kwao, nikitumaini kwamba hawatakatisha tamaa matarajio ya raia wa Taiwan,” ametangaza Hou Yuh-ih mbele ya wafuasi wake. Wakati wa hotuba yake ya kwanza, Rais Mteule Lai Ching-te amepongeza "sura mpya katika demokrasia yetu."

40.2% ya kura

Makamu wa rais anayeondoka Lai Ching-te, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (DPP), amepata asilimia 40.2 ya kura Jumamosi jioni, kulingana na takriban matokeo rasmi ya mwisho. Mpinzani wake mkuu Hou Yu-ih, 66, mgombea wa Kuomintang (KMT) ambaye anatetea uhusiano na Beijing, amepata 33.4% ya kura. Mgombea wa tatu, Ko Wen-je, 64, kutoka chama kidogo cha Taiwan People's Party (TPP) na ambaye anajionyesha kama mpinzani, ameshika nafasi ya tatu kwa 26.4%.

Wataiwan pia wamepiga kura ya kurejesha viti 113 katika Bunge. Chama cha Democratic Progressive Party (DPP) kwa upande mwingine kimepoteza wingi wake kamili huko, kulingana na mwanahabari wetu nchini Taiwan, Adrien Simorre. Kwa hivyo kitalazimika kuunda pamoja na chama cha tatu, Chama cha Meya wa zamani wa Taipei, Ko Wen-je. Chama hiki kimewashangaza wengi kwa kufanya kampeni katika masuala ya ndani, kama vile bei ya nyumba, mishahara midogo, kesi za rushwa, masuala yote ambayo yanatia wasiwasi kizazi kipya. Msimamo wake juu ya uhusiano na China bado haueleweki.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.