Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mapigano kaskazini mwa Kosovo yasababisha makumi ya watu kujeruhiwa

Makabiliano makali yamezuka Jumatatu Mei 29 kaskazini mwa Kosovo kati ya waandamanaji wa Serbia, polisi wa Kosovo na wanajeshi wa kikosi kinachoongozwa na NATO (KFOR).

Waserbia wa Kosovo wakabiliana na polisi wa kutuliza ghasia wakati wa mkutano wao wa kudai kufutwa kazi kwa mameya wapya waliochaguliwa kutoka jamii ya Albania mbele ya jengo la manispaa huko Zvecan, kaskazini mwa Kosovo, Mei 29, 2023.
Waserbia wa Kosovo wakabiliana na polisi wa kutuliza ghasia wakati wa mkutano wao wa kudai kufutwa kazi kwa mameya wapya waliochaguliwa kutoka jamii ya Albania mbele ya jengo la manispaa huko Zvecan, kaskazini mwa Kosovo, Mei 29, 2023. AFP - -STR
Matangazo ya kibiashara

Polisi ilijaribu kutawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi, gruneti, huku waandamanaji wenye hasira wakirusha mawe, chupa na vilipuzi. Mapigano makali yaliwajeruhi takriban watu 50 wa kutoka jamii ya Serbia, huku mtu mmoja kutoka jamii hiyo akipigwa risasi za moto, na angalau 25 kujeruhiwa kati ya vikosi vya Hungary na Italia vya KFOR, jeshi la NATO huko Kosovo, anaripoti mwandishi wetu huko Belgrade, Philippe Bertinchamps.

Matukio haya yalizuka, huku mvutano umekuwa ukiongezeka tangu Ijumaa, Mei 26 kati ya wakazi wa Serbia, walio wengi kaskazini mwa Kosovo, na polisi wa Kosovo. KFOR imeimarisha uwepo wake katika eneo la tukio, wakati jeshi la Serbia likiwa "katika hali ya tahadhari" karibu na mpaka wa utawala, Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amesema hivui punde siku wa Jumatatu kutoka Belgrade, ambaye amebaini kwamba "matukio mbaya huenda yakatokea".

Mameya wapingwa

Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika leo asubuhi katika maeneo manne kaskazini mwa nchi: Mitrovica Kaskazini, Zvecan, Leposavic na Zubin Potok, kupinga mameya wapya kutoka jamii ya Albania, waliochaguliwa mwezi Aprili mwaka huu wakati wa uchaguzi uliosusiwa na wapiga kura wa Serbia ambao hawatambui mamlaka ya Pristina na ni waaminifu kwa Belgrade. Ni wapiga kura 1,500 tu, kati ya takriban wapiga kura 45,000 waliojiandikisha, walishiriki.

Madiwani hawa wa jiji walitawazwa wiki iliyopita na serikali ya Albin Kurti, Waziri Mkuu wa eneo hili lenye watu wengi wa Albania, akipuuza wito wa kuwepo na utulivu uliozinduliwa na Umoja wa Ulaya na Marekani. Waandamanaji wa Serbia ambao walikuwa wamekusanyika hasa mbele ya manispaa ya Zvecan wanadai kuondolewa kwa mameya wa Albania, lakini pia kuondolewa kwa vikosi vya polisi vya Kosovo, ambavyo walikabiliana navyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.