Pata taarifa kuu

China yakaribisha luteka 'iliyofaulu' kuzunguka Taiwan

Jeshi la China limesema Jumatatu kwamba "limekamilisha kwa mafanikio" luteka yake ya kijeshi iliyolenga kuzunguka kisiwa kinachojitawa cha Taiwan kwa siku tatu, ambacho Beijing inadai kuwa ni mkoa wa China.

Mazoezi haya ambayo yamelaaniwa na Taiwan na Marekani ambayo ilitoa wito wa "kujizuia", huku ikipeleka meli kubwa ya kijeshi katika maji yanayodaiwa na Beijing kuwa ni milki yake, yamejumuisha meli kadhaa za kivita na hadi ndege 70 na hivyo kuata uungwaji mkono wa kisiasa kutoka Urusi leo Jumatatu Aprili 10.
Mazoezi haya ambayo yamelaaniwa na Taiwan na Marekani ambayo ilitoa wito wa "kujizuia", huku ikipeleka meli kubwa ya kijeshi katika maji yanayodaiwa na Beijing kuwa ni milki yake, yamejumuisha meli kadhaa za kivita na hadi ndege 70 na hivyo kuata uungwaji mkono wa kisiasa kutoka Urusi leo Jumatatu Aprili 10. AP
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Aprili 8 hadi 10, kamandi ya jeshi la China "imekamilisha kwa mafanikio kazi mbalimbali za 'maandalizi ya kijeshi' kuzunguka kisiwa cha Taiwan kwa zoezi la 'Upanga wa Pamoja', jeshi limesema katika ujumbe uliorushwa kwenye mitandao ya kijamii.

"Imejaribu kwa uwezo wake wa 'pamoja' wa kupambana katika mazingira halisi", amri ya Uchina iliongeza.

Mazoezi haya ambayo yamelaaniwa na Taiwan na Marekani ambayo ilitoa wito wa "kujizuia", huku ikipeleka meli kubwa ya kijeshi katika maji yanayodaiwa na Beijing kuwa ni milki yake, yamejumuisha meli kadhaa za kivita na hadi ndege 70 na hivyo kuata uungwaji mkono wa kisiasa kutoka Urusi leo Jumatatu Aprili 10.

Msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba "China ina haki huru ya kujibu (kwa) vitendo uchochezi" wa Marekani, "hasa ​​kwa kufanya mazoezi ya kijeshi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.