Pata taarifa kuu

China yaendelea na luteka karibu na Taiwan na kurusha risasi za moto

Luteka kubwa ya kijeshi ya China imeendelea Jumatatu hii asubuhi katika Mlango-Bahari wa Taiwan. Mamlaka katika kisiwa hicho inasema wamegundua meli 11 za kivita za China na ndege 59 karibu na Taiwan. Na kwa siku hii ya tatu mfululizo ya mazoezi ya kijeshi, zoezi la urushaji wa risasi za moto limepagwa kufanyika.

Meli ya jeshi la China wakati wa Operesheni "Common Sharp Sword" karibu na Taiwan, Aprili 8, 2023.
Meli ya jeshi la China wakati wa Operesheni "Common Sharp Sword" karibu na Taiwan, Aprili 8, 2023. © Eastern Theatre Command/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mazoezi hayo yalianza saa moja asubuhi Jumatatu hii na yatadumu hadi saa mbili usiku. Zoezi la urushaji wa risasi za moto litafanyika karibu na kisiwa cha Pingtan, kilicho mbali na mkoa wa mashariki wa China wa Fujian, kwa hiyo karibu na Taiwan, anaripoti mwandishi wetu wa Beijing, Stéphane Lagarde. Meli za abiria zimeshauriwa kuwekwa mbali na njia za majini.

Kulingana na Beijing, iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP, "ndege za kivita za China zilizobeba silaha za moto zilirusha makombora" karibu na Taiwan. Hii si mara ya kwanza kwa Jeshi la Ukombozi wa Watu (PLA) kufyatua risasi za moto kwenye Mlango wa Taiwan. Mazoezi kama hayo yalifanyika wakati wa majira ya Joto mwaka 2022, kufuatia ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani katika kisiwa hiki. Mazoezi haya wakati huo yalifanyika kwa umbali karibu na pwani ya Taiwan.

Sehemu za propaganda

Operesheni hii mpya, iliyobatizwa "Upanga mkali wa pamoja", inasambaa katika video za propaganda zenye muziki wa kijeshi na picha za ndege, boti ikiwa ni pamoja na ndege kubwa ya mwisho ya China, Shandong, ambayo ipo katika eneo hilo na wanajeshi wakitokea kwenye kambi zao. Ni suala la kuandaa "kufungwa" kwa Taiwan, hili ndilo neno lililotumiwa na mamlaka ya China asubuhi ya leo. Mazoezi haya kujibu ziara ya Tsai Ingwen nchini Marekani yanatarajiwa kuendelea Jumanne Aprili 11, Alhamisi Aprili 13, Jumamosi Aprili 15, Jumatatu Aprili 17 na Alhamisi Aprili 20.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.