Pata taarifa kuu

China yapaza sauti baada ya ziara ya rais wa Taiwan nchini Marekani

Baada ya kupeleka meli za kivita karibu na Taiwan siku ya Alhamisi na Ijumaa, Aprili 7, China inatangaza vikwazo vipya dhidi ya watu binafsi na taasisi nchini Marekani. Mkutano kati ya rais wa Taiwan na Kevin McCarthy, spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani unachukuliwa na china kama chokochoko.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning tarehe 6 Aprili 2023.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning tarehe 6 Aprili 2023. AP - Andy Wong
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Beijing, Stéphane Lagarde

China haikasiriki na inaendelea na majibu yake dhidi ya kile kinachoonekana huko Beijing kama ishara ya uchochezi. Mamlaka ilionya: kupeana mkono kwa urahisi kati ya Tsai Ing-wen na Kevin McCarthy kulichukuliwa kuwa uchochezi, na kusababisha kisasi mara moja.

Matokeo yake: taasisi mbili za Marekani zinakabiliwa na vikwazo hivi vipya vya China. Taasisi ya Hudson, ambayo ilitoa tuzo kwa rais wa Taiwan Machi 30, na Maktaba ya Ronald Reagan huko California, ambapo Tsai Ing-wen alikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani vinakabiliwa na vikwazo vya China.

Meli za kivita zatumwa karibu na Taiwan

Vikwazo hivi vinatumika kwa wafanyakazi wa mashirika haya, pamoja na mwakilishi wa Taiwan nchini Marekani, Hsiao Bi-khim. Wizara ya Mambo ya Nje ya China inathibitisha Ijumaa hii, Aprili 7 kwamba taasisi kama watu wanaolengwa sasa zimepigwa marufuku kuzungyumza, ushirikiano, biashara na watu au taasisi nchini China, Hong Kong na Macao zikiwemo.

Siku ya Alhamisi, meli tatu za kivita na helikopta zilitumwa katika eneo la Ulinzi la Taiwan. Na siku ya Ijumaa, meli tatu za kivita za China zilipitia maji yanayozunguka kisiwa hicho kinachojitawala, Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema, ikiongeza kuwa ndege ya kivita na helikopta pia ilipitia eneo hilo la Ulinzi wa Anga (Adiz) la Taiwan. Hatua kama hizo zilichukuliwa kufuatia ziara ya Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, katika msimu wa joto wa 2022.

Katika maoni yake ya kwanza ya hadharani tangu mkutano wa California, rais wa China amesema kutarajia maelewano juu ya Taiwan ni "mawazo ya kutamani". "Mtu yeyote anayetarajia China kuafikiana kuhusu suala la Taiwan itakuwa ni kama ndoto ya mwendawazimu," Xi Jinping ameongeza kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.