Pata taarifa kuu

Washington yaiuzia tena silaha Taiwan: Beijing yataka kufutwa kwa kandarasi

China imeitishia Marekani kwa kulipiza kisasi kufuatia tangazo la siku ya Ijumaa Septemba 2 la mauzo makubwa zaidi ya silaha za Marekani kwa Taiwan tangu kuwasili kwa Joe Biden katika Ikulu ya White House. Baada ya kulaani uuzaji huo, mamlaka ya China imeitka Washington isitishe mkataba huu wa dola bilioni 1.1.

Taiwan: Makombora ya Sidewinder ya Marekani yanapakiwa kwenye ndege katika kambi ya kijeshi ya Taitung (picha ya zamani ya 2018). Marekani ilitangaza mnamo Septemba 2, 2022 uuzwaji wa silaha mpya kwa kiasi cha dola bilioni moja kwa Taiwan.
Taiwan: Makombora ya Sidewinder ya Marekani yanapakiwa kwenye ndege katika kambi ya kijeshi ya Taitung (picha ya zamani ya 2018). Marekani ilitangaza mnamo Septemba 2, 2022 uuzwaji wa silaha mpya kwa kiasi cha dola bilioni moja kwa Taiwan. REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

Beijing iliziba masikio wakati Marekani ilipoiomba China kuacha kufanya biashara na Urusi kufuatia uvamizi wa Ukraine. Kwa hivyo kuna nafasi ndogo leo kwamba wito huu utasikika, licha ya hasira ya China.

Kupitia ubalozi wake mjini Washington, diplomasia ya China imetangaza "inapinga vikali" uuzaji huu mpya wa silaha, ambao unakuja mwezi mmoja baada ya ziara ya Nancy Pelosi nchini Taiwan. Ziara ya mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi ilikuwa ilisababisha China kufanya mazoezi ya kijeshi ambayo hayajawahi kufanywa katika Mlango wa Formosa.

Kwa upande wa China, hofu ya kuzingirwa inakumbushwa katika kila hotuba. Mamlaka ya Kikomunisti pia ililaani wiki hii kuboreshwa kwa mfumo wa ulinzi wa makombora wa mwinuko wa Marekani (THAAD) huko Korea Kusini na kuendelea kwa kujiimarisha kwa silaha kwa vikosi vya kujilinda vya Japani.

Lakini suala nyeti zaidi kwa Beijing bado ni Taiwan. Mamlaka ya Kikomunisti inachukulia eneo hilo kama moja ya maeneo ya China lililoasi ambalo linahitaji kuunganishwa tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.