Pata taarifa kuu

Kikao cha G20: Urusi na China zalaani 'vitisho' vya nchi za Magharibi

Moscow na Beijing zimeshutumu nchi za Magharibi kikao cha kundi la chi zilizostawi kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi, G20, siku ya Alhamisi kwa kutumia "maneneo yasiyofaa" na "vitisho" kulazimisha maoni yao, wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa kundi hilo wakikutana India, wakigawanyika kwa vita vya Ukraine.

Ishara ya mgawanyiko ndani ya G20, mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken ameonya kuwa hana mpango wa kukutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje.
Ishara ya mgawanyiko ndani ya G20, mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken ameonya kuwa hana mpango wa kukutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje. REUTERS - AMIIT DAVE
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa diplomasia ya Urusi Sergei Lavrov amethibitisha, Alhamisi, Machi 2, kwamba hakuna taarifa ya pamoja itatolewa mwishoni mwa mkutano wa mawaziri wa G20 nchini India na kuzishutumu nchi za Magharibi kwa kushindwa kuafikiana.

"Tunazungumza juu ya tabia njema. Naam, wenzetu wa Magharibi wamekuwa wabaya zaidi. Hawafikirii kuhusu diplomasia tena, wanafanya udanganyifu na kutishia kila mtu," Sergei Lavrov amewaambia waandishi wa habari.

Ishara ya mgawanyiko ndani ya G20, mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken ameonya kuwa hana mpango wa kukutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje.

Kando ya mkutano huu, Sergei Lavrov alizungumza na mwenzake wa China Qin Gang, ambaye nchi yake ina uhusiano wa karibu na Moscow.

Wawili hao 'walikataa kwa kauli moja majaribio ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, kuweka mbinu za upande mmoja kupitia ulaghai na vitisho', kulingana na taarifa kutoka diplomasia ya Urusi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.