Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Kyiv yapokea msaada wa kwanza kuhusiana na mfumo wa ulinzi wa angani

Ukraine imepokea mfumo wake wa kwanza wa ulinzi wa angani. Mfumo huo umeotolewa na Ujerumani na ambao utatumiwa kwa ulinzi wa jiji kubwa la Kyiv dhidi ya mashambulizi ya anga. Wakati huo huo, Mawaziri thelathini wa Ulinzi wa NATO wanakutana mjini Brussels Jumatano hii na Alhamisi ili kubaini msimamo wao katika kukabiliana na hali hii mpya kati ya Moscow na Kyiv.

Voiture en feu après une attaque russe à Kiev, en Ukraine, le lundi 10 octobre 2022.
Voiture en feu après une attaque russe à Kiev, en Ukraine, le lundi 10 octobre 2022. AP - Roman Hrytsyna
Matangazo ya kibiashara

Mfumo huu wa ulinzi wa angani ni hatua ya kwanza tu, zingine tatu zitawasilishwa katika miezi ijayo, amesema Christine Lambrecht, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani. Iris-T ni mfumo wa ulinzi wa angani wenye uwezo wa kutoaulinzi katika eneo lenye kilomita 40, na tangu Jumatatu, wakati mvua ya makombora ya Urusi ylianguka kwenye miji ya Ukraine, mifumo hii ya ulinzi hadi imekuwa kipaumbele namba moja cha Kyiv.

Marekani pia inaahidi kutoa msaada wake

Mashambulizi haya katika kina cha eneo la Ukraine ni mabadiliko ya kweli katika mkakati wa Urusi. Moscow, kwa kuzindua upya msururu wa mashambulio ya makombora ya uso kwa uso, kama ilivyokuwa ikifanywa katika siku za mwanzo za mzozo, sasa inatishia miundombinu ya kiraia ya Ukraine katika miji iliyo mbali na maeneo ya mapigano, kama Lviv upande wa magharibi, ambayo ilikuwa haijakumbwa na mashambulizi yoyote kufikia sasa.

Marekani imeahidi mifumo ya ulizi wa makombora ya Nasam: miwili mwanzoni, kisha mingine sita siku zijazo. Ukraine pia inaangalia mifumo ya Ufaransa ya SAMP-T Mamba inayotengenezwa na kampuni za Thalès na MBDA, lakini majeshi ya Ufaransa yana mifumo minane tu kati ya mifumo hii, mifumo ambayo pia ni ngumu kuitumia.

Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakutana Brussels

Huu ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa Muungano wa Atlantic tangu mashambulizi mapya ya Urusi katikati ya miji ya Ukraine: Mawaziri thelathini wa Ulinzi wa NATO wanakutana mjini Brussels Jumatano na Alhamisi kubainisha msimamo wao katika kukabiliana na ongezeko hili jipya la mashambulizi. Katikati ya mijadala yao ni ulinzi wa anga wa Ukraine, anaripoti mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet.

Ulinzi wa angani wa Ukraine ni "kipaumbele" cha washirika thelathini, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesisitiza leo Jumatano. Hili ni jibu la moja kwa moja kwa ombi lililotolewa Jumatatu asubuhi na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Matarajio ya Katibu Mkuu wa NATO ni kuona nchi nyingine zikijitolea kusambaza silaha, hata kama Muungano wa Atlantic uko nyuma kidogo katika suala hili, kwa sababu ni nchi washirika ambazo zinapaswa kuamua kwa upande wao kile wanacho.

Suala jingine la siku hiyo litakuwa ongezeko la uzalishaji wa viwanda vya ulinzi, kwa sababu usambazaji wa silaha kwa Ukraine unapunguza hatari ya hifadhi ya zana za kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.