Vita nchini Ukraine: Utulivu warejea na hofu ya mashambulizi mapya ya Urusi yatanda Kyiv
Jumatatu hii, Oktoba 10, Moscow ilirusha makombora zaidi ya 80 katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, lakini pia katika miji mingine mikubwa ya Ukraine, Ternopil, Dnipro, Lviv na Kharkiv.
Imechapishwa:
Takriban watu 19 waliuawa na mashambulizi hayo siku ya Jumatatu na 105 kujeruhiwa, kulingana na ripoti mpya iliyotangazwa Jumanne na mamlaka, katika mashambulizi haya ambayo pia yalilenga miundombinu ya nishati. Kwa upande wa mamlaka, wamesema Urusi inaweza kuendelea kushambulia mtambo wa umeme nchini Ukraine.
Katika kipindi cha saa chache kumeshuhudiwa mawimbi na mawimbi ya milipuko, sio yu hapa mjini Kiev, lakini pia katika maeneo mbali mbali ya nchi hii, kutoka Lviv magharibi mwa Kharkiv mashariki mwa ina Odesa katika kusini.
Ni vigumu kuelezea ni wapi kunalengwa, lakini taarifa kutoka katika wizara ya utamaduni ya Ukraine inasema majumba ya makumbusho na muziki yamepigwa kwa makombora.
Wakati huo huo, Jumanne asubuhi, jeshi la Urusi kwa mara nyingine tena lilishambulia mji wa Zaporizhia, ambapo maeneo ya makazi ya watu yalipigwa kwa bomu.