Pata taarifa kuu

Rais wa Ukraine atoa wito kwa ujumbe wa uchunguzi kwenye mpaka wa Belarus

Mashambulio ya mabomu ya Urusi nchini Ukraine yalikuwa kwenye ajenda ya mazungumzo ya nchi za uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni G7, ambazo zimekutana kwa dharura na kwa njia ya video mnamo Jumanne, Oktoba 11. Volodymyr Zelensky alijiunga na mazungumzo hayo, mwanzoni mwa mkutano, kama mgeni. Fursa kwa rais wa Ukraine kutoa maoni yake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ahudhuria mkutano wa dharura wa viongozi wa G7 huko, Berlin, Ujerumani, Oktoba 11, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ahudhuria mkutano wa dharura wa viongozi wa G7 huko, Berlin, Ujerumani, Oktoba 11, 2022. REUTERS - BPA
Matangazo ya kibiashara

Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa wanachama wa G7 kusaidia kupata mfumo wa kuzuia makombora na mabomu kwenye anga yake kukabioliana na mashambulizi ya angani.

"Ni muhimu kwamba tuwe na idadi ya kutosha ya makombora kwa ulinzi wa anga na ulinzi wa makombora na kwamba yaunganishwe na mifumo yetu ya ulinzi," rais wa Ukraine amesisitiza.

Joe Biden, ambaye amezungumza na mwenzake wa Ukraine Jumatatu jioni, tayari ameahidi kwamba Marekani itaipatia Ukraine mifumo ya hali ya juu ya ulinzi wa anga, kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Marekani. Ujerumani pia itawasilisha haraka mfumo wa kwanza wa ulinzi wa anga ulioahidiwa kwa muda mrefu. Canada itatuma wahandisi 40 wa ziada kusaidia Poland katika mpango wake wa mafunzo kwa vikosi vya Ukraine.

Kyiv pia ina wasiwasi kuhusu matukio yanayotokea upande wa pili wa mpaka wake wa kaskazini, huko Belarus, baada ya tangazo la Jumatatu la kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha kijeshi na Urusi.

Volodymyr Zelensky anashutumu Moscow kwa kutaka "kuivuta Belarusi kwenye vita". Anatoa wito wa kuanzishwa kwa ujumbe wa kimataifa wa uchunguzi kwenye mpaka kati ya Ukraine na Belarus, "kufuatilia hali ya usalama katika eneo hilo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.