Pata taarifa kuu

Ukraine: Takriban raia 17 wauawa baada ya kushambuliwa kwa makombora Zaporizhia

Vikosi vya jeshi la Urusi vimefanya mashambulizi katika mji wa Zaporizhia, kusini-mashariki mwa Ukraine. Usiku wa Jumamosi Oktoba 8 kuamkia Jumapili Oktoba 9, mji wa sita wa nchi hiyo ulikumbwa tena na mashambulizi makubwa ya mabomu yaliyoua raia 17 katika eneo la makazi.

Moja ya majengo yaliyoharibiwa baada ya shambulio la Urusi huko Zaporizhia, Oktoba 6, 2022.
Moja ya majengo yaliyoharibiwa baada ya shambulio la Urusi huko Zaporizhia, Oktoba 6, 2022. AFP - MARINA MOISEYENKO
Matangazo ya kibiashara

Majira ya saa mbili asubuhi, makombora kumi ya Urusi yaliangukia mji wa Zaporijja, na kusababisha uharibifu mkubwa sana katikati ya eneo la makazi.

Majengo matano yaliharibiwa kabisa na mengine takriban arobaini kuathiriwa vibaya. Idadi ya waliofariki kwa muda ni 17 na wengine kadhaa kujeruhiwa, wakati waokoaji bado wanatafuta waathiriwa chini ya vifusi.

utawala wa kigaidi

Hali ni ngumu kwa wakazi wa mji wa Zaporizhia, kwani Jumapili hii mamia ya wakazi wanajaribu kuondoka katika jiji hilo, ambalo sasa linakumbwa na mashambulizi ya mabomu kila mara.

Mnamo Septemba 30, vikosi vya Urusi vifyatua kombora dhidi ya msafara wa magari, na kuua raia 30, wakati siku ya Alhamisi kombora lilianguka katika barabara kuu ya jiji hilo, na kuua jumla ya watu 17.

Wakati Moscow haidhibiti mji mkuu huu wa eneo ambalo imeamua kuunganisha, inaonekana kwamba jeshi la Urusi limeamua kuweka serikali ya ugaidi katika mji wa Zaporizhia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.