Pata taarifa kuu

Nagorno-Karabakh: Armenia yawataka walinda amani wa Urusi kuchukua hatua

Kufuatia kuzuka upya kwa ghasia huko Nagorno-Karabakh, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian amelihutubia taifa asubuhi ya Agosti 4, na  ametoa wito kwa walinda amani wa Urusi waliotumwa katika eneo hili linalozozaniwa kuchukua hatua.

Waziri Mkuu wa Armenia, hapa akiwa mji mkuu Yerevan, mnamo Julai 17, 2021.
Waziri Mkuu wa Armenia, hapa akiwa mji mkuu Yerevan, mnamo Julai 17, 2021. AFP - KAREN MINASYAN
Matangazo ya kibiashara

Nikol Pashinian sasa anaiomba Urusi, kwa njia ya moja kwa moja: "Kuna mstari wa mawasiliano ambapo walinda amani huwekwa, na eneo hili liko chini ya wajibu wao". Shirika la habari la Urusi Interfax limebaini hili: kwa upande wa Waziri Mkuu wa Armenia amesema askari hawa ni "wana umuhimu mkubwa katika usalama wa Waarmenia wa Nagorno-Karabakh" lakini "mfululizo wa matukio ambayo yamefanyika tangu mwezi Novemba 2020 (Nikol Pashinyan anazungumza juu ya vita na matukio yaliyofuata) yanaibua maswali katika jamii ya Waarmenia kuhusu maudhui na kiini cha kazi ya kulinda amani”.

Waziri Mkuu ametoa wito wa "ufafanuzi" wa operesheni ya ulinzi wa amani. Kupitia sauti ya msemaji wake, Kremlin imesema siku ya Alhamisi "kutiwa wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama karibu na Nagorno-Karabakh" na kutoa wito kwa pande husika "kujizuia". Dimitri Peskov ambaye "hakatai" kuwa suala hilo litajadiliwa Ijumaa Agosti 5 kati ya Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan. Viongozi hao wawili wanakutana tena katika makazi ya Rais wa Urusi majira ya kiangazi.

Siku ya Jumatano, rais wa jamhuri iliyojitangaza ya Karabakh aliagiza wanaume wa eneo hilo kuhamasishwa kushirikiana na vyomvo vya usalama na jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.