Pata taarifa kuu

Ufilipino: Kimbunga Megi chaua takriban watu 58

Maporomoko ya udongo na mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Megi yamegharimu maisha ya watu 58 nchini Ufilipino, kulingana na ripoti rasmi za hivi punde zilizotolewa leo Jumatano. Vifo vingi vilitokea karibu na mji wa Baybay katika mkoa wa kati wa Leyte, ambapo vijiji kadhaa vikifunikwa ma matope.

Afisa wa kikosi cha Ulinzi wa Pwani nchini Ufilipino akiwa amembeba msichana mdogo walipokuwa wakitembea kwenye barabara iliyofurika maji, baada ya dhoruba ya kitropiki ya Megi kupiga, katika mkoa wa Leyte, Ufilipino Aprili 10, 2022.
Afisa wa kikosi cha Ulinzi wa Pwani nchini Ufilipino akiwa amembeba msichana mdogo walipokuwa wakitembea kwenye barabara iliyofurika maji, baada ya dhoruba ya kitropiki ya Megi kupiga, katika mkoa wa Leyte, Ufilipino Aprili 10, 2022. © via REUTERS - PHILIPPINE COAST GUARD
Matangazo ya kibiashara

Waokoaji wanaendelea kuondoa matope kutafuta waathiriwa katika vijiji vyenye wakaazi wa maisha duni katikati mwa Ufilipino, ambapo takriban watu 59 wameangamia katika maporomoko ya mawe makubwa yaliyosababishwa na Kimbunga Megi.

Takriban watu watano wamefariki dunia katika eneo la Pilar, kijiji cha pwani chenye watu 400 katika mkoa wa kati wa Leyte, polisi imesema.

Nyumba nyingi zimesombwa hadi baharini kwa maporomoko makubwa ya udongo.

Ara Mae Canuto, 22, alikuwa nyumbani kwa familia yake huko Pilar aliposikia kelele "kama helikopta" ikitokea. Alijaribu kukimbia, lakini alijikuta akinaswa na maji ya matope na karibu kuzama.

"Masikio yangu na pua yangu vilijaa tope," ameliambia shirika la habari la AFP kwa simu kutoka hospitali ambako anatibiwa. Baba yake amefariki duia, na mama yake hajulikani aliko.

Walipowasili kwa boti huko Pilar, barabara za kuingilia zikiwa zimekatika, waokoaji waliwahamisha karibu manusura hamsini hadi mji jirani wa Abuyog.

"Maafa haya yananivunja moyo," ameandika kwenye Facebook Lemuel Gin Traya, meya wa manispaa ya Abuyog, ambayo Pilar ni sehemu yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.